Thursday, May 19, 2016

MABAKI YA NDEGE YA EGYPT AIR YAPATIKANA

Mabaki ya ndege ya EgyptAir yapatikana

Duru za kampuni ya ndege ya EGYPTAIR zimesema kuwa wizara ya usafiri wa anga nchini humo imepokea barua rasmi kutoka kwa wizara ya maswala ya kigeni nchini Misri inayothibitisha kupatikana kwa mabaki ya ndege iliotoweka ya MS 804 karibu na kisiwa cha Karpathos.
Hivyobasi kampuni hiyo imetuma salamu za rambi rambi kwa familia za abiria na wafanyikazi waliokuwa wakiabiri ndege hiyo.
Tayari familia za abiria hao pamoja na wafanyikazi wameelezewa kuhusu tukio hilo jipya.
Kwa sasa kundi la wachunguzi wa Misri wakishirikiana na wenzao wa Ugiriki wanaendelea kutafuta mabaki mengine ya ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa imepaa kutoka uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle, Paris ikiwa na raia 15 wa Ufaransa.
Ndege hiyo pia ilikuwa na raia 30 wa Misri, raia 2 wa Iraq na raia mmoja mmoja kutoka Uingereza, Canada, Ubelgiji, Kuwait, Saudi Arabia, Algeria, Sudan, Chad na Ureno.Awalia rais wa Ufaransa Francois Hollande alikuwa amesema kuwa ndege hiyo ilianguka.

No comments:

Post a Comment