Friday, May 27, 2016

KALI YA DUNIA

Klabu ya soka yafungwa mabao 44 Ecuador

Pelileo Sporting Club
Klabu moja ya soka nchini Ecuador imepata ushindi mkubwa ambao ukiidhinishwa basi itakuwa rekodi mpya ya ufungaji mabao duniani.
Klabu hiyo ya Pelileo Sporting Club ilicharaza Indi Native mabao 44-1 katika mechi ya ligi ya daraja la tatu nchini humo mbele ya mashabiki 200.
Mshambuliaji wa Pelileo Ronny Medina alifunga mabao 18.
Rais wa Indi Native Diego Culequi amesema matokeo hayo hayakutarajiwa na wachezaji hawakuwa wamezoea joto kali ambalo anasema lilichangia kushindwa kwao.
Mwandishi wa habari Mwingereza Tim Vickery, ambaye amekuwa Brazil kwa miaka 20, amesema Bon Accord kwa sasa wamejadiliwa sana katika vyombo vya habari Ecuador.
Anasema ligi ya daraja la tatu ya Ecuador huwa na ushindani mkubwa.
Rekodi ya sasa inashikiliwa na Arbroath FC ya Scotland iliyofunga mabao 36-0 dhidi ya Bon Accord miaka 131 iliyopita.
Mwenyekiti wa Arbroath FC John Christison amesema ana wasiwasi kiasi kwamba rekodi yao waliyoiweka 1885 huenda ikavunjwa.
Amesema klabu hiyo itasubiri uamuzi wa Guinness World Records.

No comments:

Post a Comment