Monday, May 23, 2016

MAANDAMANO KENYA YAZIMWA

Upinzani waandamana tena Kenya

Uchaguzi
Muungano wa upinzani nchini Kenya CORD Umefanya maandamano katika miji mikuu nchini humo kuwashinikiza maafisa wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) kujiuzulu.
Viongozi wa muungano huo wamesema maafisa hao hawawezi kuandaa uchaguzi huru na wa haki mwaka ujao.
Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na marungu kutawanya maandamano sawa na hayo Jumatatu wiki iliyopita.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu walisema polisi walitumia nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano hayo.
Chanzo BBC
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapatangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment