Monday, May 23, 2016

WASAFIRI MABASI YAENDAYO MIKOANI WALALAMIKA



Tangakumekuchablog
Tanga, WASAFIRI wa mabasi yaendayo Mikoani Tanga wameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Safari za Nchi Kavu na Majini( Sumatra) kupunguza nauli baada ya mafuta kushuka bei.
Wakizungumza na waandishi wa habari kituo cha Mabasi cha Kange  yaendayo Mikoani na Wilayani , wasafiri hao wamesema mbali ya bei ya mafuta kushuka nauli imepanda maradufu.
Wamesema kipindi hiki cha  likizo kwa wanafunzi shuleni kimekuwa kikiwanyima wanafunzi fursa  kwenda kwa wazazi wao baada ya nauli kuongezeka maradufu.
Wamesema mbali ya nauli hizo za mabasi pia nauli za daladala na magari yaendayo Wilayani nayo  zimekuwa zikiongezeka bila kufuata bei elekezi za Sumatra.
Wameitaka Serikali kupitia Sumatra kusimamia bei hizo na kuondosha mizozo kwa abiria na wamiliki wa mabasi na kuwa na bei za aina moja .
                                                  Mwisho

No comments:

Post a Comment