Saturday, May 28, 2016

WHO LAONDOA HAFU UGONJWA WA ZIKA OLIMPIC

 WHO laondoa wasiwasi  Olimpiki

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa limeingilia kati katika kukabiliana na virusi vya Zika huku kukiwa na wito kwa mashindano ya michezo ya Olimpiki kuahirishwa kufuatia mlipuko wa virusi hivyo.
Afisa wa WHO Bruce Aylward ameiambia BBC kwamba hatua za kukabiliana na ugonjwa huo zimekamilishwa.
a
Alikiri kwamba shirika la afya duniani WHO linaweza kufanya kazi nzuri zaidi kupitia kutoa tangazo kuhusu kile kinachoendelea na kwamba hakuna haja ya kuahirisha michezo hiyo.
Katika barua ya wazi wanasayansi 152 walisema kuwa utafiti waliofanya kuhusu Zika umeonyesha kuwa ni hatari kwa michezo hiyo kuendelea.
Pia wamesema kuwa shirika hilo la afya duniani linafaa kufuata maelezo yake kuhusu Zika.
Ugonjwa huo unahusishwa na watoto walio na vichwa vidogo na ubongo uliodumaa.
BBC

No comments:

Post a Comment