Friday, May 27, 2016

ANG'ATWA NA NYOKA WAKATI AKIENDA HAJA CHOONI

Ang'atwa uume na nyoka Thailand

Raia mmoja wa Thailand anaendelea kuuuguza jeraha katika hospitali moja baada ya nyoka aina ya chatu kutokea ndani ya choo na kumng'ata uume wake.
Madaktari wanasema kuwa Attaporn ambaye alipoteza damu nyingi anaendelea vyema na matibabu.
Wafanyikazi walilazimka kukiharibu choo hicho.Baadaye nyoka huyo aliachiliwa na kuingia msituni.
Kisa hucho kilitokea wakati ambapo Attaporn mwenye umri wa miaka 38 alielekea katika choo chake nyumbani kwake huko Chachoengsao,mashariki mwa Bangkok kabla ya kwenda kazini siku ya Jumatano.
Wakati alipokuwa akitumia choo hicho alihisi kung;atwa na kitu na kupata maumivu mkali.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment