Friday, May 27, 2016

JINO LA NYANGUMI ALIEISHI MIAKA MILIONI TANO LAPATIKANA

Jino kubwa la nyangumi lapatikana Australia

Jino kubwa la nyangumi limepatikana ufukweni Australia, na kuwa thibitisho la kwanza kwamba nyangumi wakubwa hatari sana waliishi mbali na Amerika.

Mkusanyaji wa visukuku Murray Orr alipata jino hilo lenye urefu wa sentimeta 30 (inchi 12) ufukweni Beaumaris Bay karibu na mji wa Melbourne mwezi Februari.

Alilikabidhi kwa makumbusho ya Victoria, ambayo yalianza kulionesha kwa umma Alhamisi.

Inakadiriwa kwamba nyangumi mwenye jino hilo aliishi zaidi ya miaka milioni tano iliyopita. Alitoka kwa aina ya nyangumi ambao siku hizi hawapatikani duniani.

Nyangumi hao wanaaminika kuwa watangulizi wa nyangumi wakubwa wa sasa wajulikanao kwa Kiingereza kama "sperm whales".

No comments:

Post a Comment