Maryam Abrahman (kushoto) akionyesha
mkono wa mume wake, Abdalla Nassir, wakazi wa kijiji cha Mtimbwani Wilayani
Mkinga Mkoani Tanga wenye makovu
uliopata kilema baada ya kung’atwa na kuku na kumsababishia kilema cha mkono
kupinda.
Kijana huyo mwenye ndoto ya maendeleo alipatwa na mkasa huo na kwa sasa amepata kilema cha mkono wa kushoto ambao umepinda na haufanyi kazi ya aina yoyote.
Akisimulia mkasa huo kwa umakini na utulivu alisema alishangazwa na kuku huyo kumdonoa ambapo hakusikia maumivu yoyote zaidi ya ubaridi ambao ulimshangaza.
Alisema ubaridi huo ulidumu kwa hadi siku ya pili asubuhi wakati alipoamka na kusikia maumivu ambayo familia yake na yeye pia walishangaa.
Aliongeza na kusema kuwa wakati wa kutafuta tiba alipanda milima na mabonde na mwisho kugundua kuku huyo hakuwa kuku wa kawaida.
Alibainisha na kuongeza kuwa kama kuku huyo angemchelewesha kidogo kumuuza angelimuweka na kila siku angemuliza "Kwanini amenipatia kilema cha maisha"
No comments:
Post a Comment