ZULIA LA FAKI
NILIKIONA CHA MTO URITHI
WA BABU 13
ILIPOISHIA
Kama vile magoti
yalimnyong’onyea, mzee alirudi ghafla kwenye kiti chake.
“Kwanini ninakuchanganya mzee
wangu?” nikamuuliza kwa sauti tulivu nikiwa sijui nililokuwa ndani ya moyo wa mzee huyo..
“Mimi ndiye Sharif Nasri. Huyu
ni binti
yangu na alishakufa miaka mitano iliyopita!”
Kauli ya yule mzee
ikanishitua na mimi.
“Umesema alishakufa miaka mitano
iliyopita?” nikamuuliza.
“Ndiyo alishakufa. Hivi sasa
ni marehemu. Uliponiambia ni huyu umenichanganya sana”
“Kama alishakufa miaka mitano
iliyopita, mbona nimemuona na ameniambia nije kumuulizia hapa?”
Nikaona mama mmoja na binti mmoja
aliyekuwa amefanana na Ummy, wakitoka pale barazani. Pengine ni baada ya
kusikia yale maneno.
“Kuna nini?” Yule mama
akauliza.
SASA ENDELEA
“Huyu kijana amekuja na
habari za kushangaza kidogo” Yule mzee alianza kumueleza.
“Kwani yeye ni nani?”
“Sikiliza nikueleze. Yeye
amekuja kumuulizia Ummy”
Yule mama akanitazama kisha
akaurudisha uso wake kwa yule mzee.
“Yeye hajui kama Ummy hivi
sasa ni marehemu? Amekuja kutukumbushia
msiba tuliokwishausahau”
“Anasema alikutana naye na
alimuagiza aje hapa nyumbani!”
“Alikutana naye lini?” Yule
mama aliuliza kwa mshituko.
“Eti mlikutana llini??” Yule mzee akaniuliza.
“Nilikkutana naye jana na leo
niliongea naye asubuhi kwa simu” nikamjibu.
Mama akatikisa kichwa.
“Huyo siye Ummy. Ummy
alikwishakufa mmika mitano iliyopita” Mama alisema.
“Nimemuonesha hii picha ya
marehemu. Ameniambia Ummy aliyekutana naye ndiye huyo”
“Haiwezekani. Huyo aliyekutana
naye si Ummy”
Yule msichana aliyetokana yule mama akanitazama.
“Umesema uliongea naye kwenye
simu leo?” akaniuliza.
“Ndiyo niliongea naye”
“Ulimpigia au alikupigia?”
“Alinipigia yeye”
“Hebu tuoneshe namba yake”
Nikatoa simu yangu na kuitafuta
namba aliyonipigia yule msichana,
nikamuonesha.
Msichana aliisoma ile namba kisha akagutuka.
“Mama hii ndiyo iliyokuwa
namba ya marehemu dada!” akasema kwa sauti ya
kutaharuki.
“Kwani unaikumbuka
vizuri?”Yule mama akamuuliza.
“Naikumbuka” Msichana alisema
na kurudia kuitaja ile namba kwa kuikariri
kisha akaongeza.
“Ni namba ya marehemu kweli”
Nyuso za watu wote watatu
zikawa zimebadilika. Nilijuta kufika pale nyumbani na kukuta niliyoyakuta.
“Hebu tueleze vizuri unajuana
naye vipi huyu Ummy?” Yule mama akaniuliza.
Ikanibidi nieleze ukweli wote
tangu babu yangu alipofariki mpaka
nikaenda katiika nchi nilizokwenda
kufuatilia madeni ya babu. Nikaeleza jinsi msichana huyo alivyowaua watu niliowafuata katika kila nchi
niliyokwenda. Na mtu wa mwisho aalimuua Dar es
Salaam mara tu niliporudi kutoka Afrika Kusini.
Niliwaeleza kwamba niliporudi nilimuona huyo msichana akishuka kwenye ndege akiwa
amefuatana na mtu mmoja.
“Niliwafuatilia hadi Mbezi
ambako niliona wakiingia katika
nyumba moja. Siku ya piili yake nikaona
kwenye vyomba vya habari yule mtu
ameuawa na alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wanadaiwa na babu yangu”
Mama alitoa mguno mzito
akamtazama yule binti kisha akamtazama yule mzee ambaye nilikwisahisi kuwa
alikuwa mume wake.
“Huyu kijana amekuja na
habari kubwa” akawambia kisha akanitazama na kuniuliza.
“Sasa mlikutana wapi na huyu
msichana mkiwa hapa Dar”
“Tulikutana jana. Sijui
alipataje namba yangu akanipigia simu…”
“Wewe ulijuaje kuwa ni yeye
aliyekupigia simu?”
“Sikujua kama alikuwa yeye.
Aliniambia nimfuate katika hoteli moja pale
Masaki, akaniambia alikuwa na taarifa kuhusu mali za babu yangu. Nikafika hapo hoteli. Nikaingia katiika chumba alichoniambia ananisubiri.
“Nilipoingia humo chumbani nikamuona
yeye. Kwa vile nilivyojua kuwa ndiye aliyeua wale watu, nilidhani alitaka kuniua na mimi nikatoka mbio bila
kumsikiliza. Niliporudi nyumbani alinipigia simu akaniuliza kwanini
nilimkimbia”
Niliendelea kuwaeleza jinsi
nilivyojibizanana na msichana huyo hadi
akanitajia jina lake na ubinti wake na akanitaka nifike nyumbani kwao
Mwananyamala ili nionane naye.
“Namba ya nyumba hii alikutajia yeye?”
“Ndiyo alinitajia yeye. Jana
sikufika. Leo asubuhi akanipigia simu na
kunisisitiza kuwa nifike kumuulizia. Ndio nikafika na kukutana na huyu mzee
hapa”
Palipita kimya cha karibu
robo dakika. Wenyeji wangu hao walikuwa wameduwaa wakinitazama. Sikuweza kujua
walikuwa wananiwazia nini.
Nikahisi kijasho chembamba
kikinitiririka kwenye mfereji wa uti wa mgongo wangu.
Nilikuwa nikijiuliza kama ule
ulioua watu Botswana, Zimbabwe na Afrika Kusini uulikuwa ni mzuka wa Ummy na
kwamba nilikutana na kuzungumza na
mzuka?
Maswali hayo yalikuwa
yakipita akilini mwangu kimya kimya huku nikikabiliwa na kazi ya kukwepa macho ya wale wazee waliokuwa
wakinitazama.
Ni vyema niseme ukweli kwamba
wakati ule tunazungumza, miguu yangu ilikuwa inatetemeka kwa hofu.
ITAENDELEA kesho hapahapa Usikose uhondo huu
No comments:
Post a Comment