Thursday, April 20, 2017

JIWE KUBWA LAPITA SALAMA KARIBU NA DUNIA

Jiwe hilo lilikuwa na ukubwa sawa na wa GilbratarAsteroidi kubwa ambayo inakadiriwa kuwa na ukubwa karibu sawa na wa wa Jiwe la Gibraltar imepita salama karibu na Dunia.
Asteroidi hiyo ambayo inakadiriwa kuwa na kipenyo cha karibu kilomita moja, ilipita karibu na dunia umbali wa mara tano hivi umbali kati ya Dunia na Mwezi.
Jiwe hilo ambalo limepewa jina 2014 JO25, ndilo kubwa zaidi kupita karibu na dunia tangu 2004.
Wataalamu wa anga za juu walisema fursa nzuri zaidi ya kutazama asteroidi hiyo angani itatokea Jumatano usiku.
BBC

No comments:

Post a Comment