
Vinara wa ligi kuu ya England,
Chelsea wamendeleza wimbi la ushindi katika ligi hiyo baada ya
kuichapa Manchester City kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye
dimba la Stanford Bridge.Arsenal wakicheza katika uwanja wao wa Emirate waliwachapa West Ham kwa mabao 3-0 na hivyo Arsenal kurejea katika nafasi ya tano.
Liverpool wakashindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kukubalia sare ya mabao ya 2-2 na AFC Bournemouth, Hull City wao wakashinda kwa mabao 4-2 dhidi ya Middlesbrough.
Tottenham Hotspur wakicheza ugenini katika dimba la Libery waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Swansea City, Southampton wakashinda kwa 3 - 1 dhidi ya Crystal Palace.
No comments:
Post a Comment