Tanga, MCHUNGAJI Kanisa la Sabato Centrol Tanga, Jackson Mdingi, ameitaka
jamii kudumisha upendo na mshikamano pamoja na kuwa na huruma watu wasiojiweza.
Akizungumza
mara baada ya kufanya usafi wa mazingira kwa ushirikiano na jeshi la polisi
kutoka ofisi ya kamanda wa polisi pamoja na viongozi wa dini jana, Mdingi
alisema amani iliyipo inafaa kuenziwa.
Alisema jamii
inatakuwa kulikumbuka kundi la watu wasiojiweza kwa kuwapa misaada mbalimbali
ikiwemo vyakula na kufanya usafi katika maeneo yao.
“Hapa tupo
makundi mbalimbali yakiwemo viongozi wa dini na maofisa wa polisi pamoja na
wawakilishi wa madhehebu ya dini, huu ni udhihirisho kuwa tuko wamoja hivyo
tuuenzi” alisema Mdingi
Aliwataka
viongozi wa dini kuwa na ada ya kuandaa matamasha na makongamano ambayo yatashirikisha makundi mbalimbali ya
dini jambo ambalo litawawezesha kubadilisha mawazo na kudumisha umoja.
Kwa upande
wake, Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Benedickti Wakulyamba, alisema jeshi hilo
litahakikisha linalinda watu na mali zao pamoja na kuendeleza msako wa wauzaji
wa mihadarati ikiwemo mirungi.
Alisema
wameunda kikosi maalumu ya kupambana na wapitishaji wa madawa ya kulevya na
mali za magendo katika njia za panya zikiwemo za baharini.
“Jeshi la
polisi liko makini na tumefanikiwa kuzuia mianya ya upitishaji wa madawa ya
kulevya ikiwemo mirungi, kwa sasa tunafanya msako wa watumiaji kwa kuwafuata
wanakokula” alisema Wakulyamba
Nae Diwani wa
kata ya Mzizima, Fredick Chales amezitaka taasisi nyengine za dini kuiga mfano
wa kanisa la Sabato kwa kufanya kazi za
kijamii kwa pamoja.
Alisema
kufanya hivyo itasaidia kuleta mshikamano na umoja na kuondosha matabaka ambayo
yanayoweza kuwagawa wananchi jambo ambalo halitakikani kutokea.
Maofisa Afya jiji wakijimuika na wakazi wa jiji la Tanga kufanya usafi wa mazingira kijijic ha miaka 21 .
No comments:
Post a Comment