Monday, April 3, 2017

ARSENAL WENGER LICA YA SHINIKIZO, AWASIFU WASHABIKI WA ARSENAL

ArsenalMeneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema mashabiki wa klabu hiyo walikuwa wazuri sana wakati wa mechi dhidi ya Manchester City ambayo iliisha kwa sare ya 2-2 uwanjani Emirates.
Amesema hayo licha ya kwamba bado wapo mashabiki walioandamana kumpinga wakati wa mechi hiyo ya Jumapili.
Wenger, ambaye anakabiliwa na shinikisho baada ya kushindwa mechi moja pekee kati ya sita walizocheza karibuni amekuwa akitakiwa na baadhi ya mashabiki ajiuzulu.
"Lazima niseme kwamba, licha ya yote yaliyofanywa na baadhi ya mashabiki, mashabiki wetu walikuwa wazuri sana leo," alisema Mfaransa huyo baada ya mechi.
Arsenal, ambao wameshuka hadi nafasi ya sita kwenye Jedwali, walitoka nyuma mara mbili kulazimisha sare hiyo dhidi ya vijana hao wa Pep Guardiola.
"Katika nyakati ngumu sana, tukiwa 1-0 chini na 2-1 chini, wangetugeuka lakini nafikiri walikuwa wazuri sana na walituwezesha kupitia vipindi hivyo vigumu."
BBC

No comments:

Post a Comment