Tuesday, April 18, 2017

WANAFNZI 105 WANASOMA CHUMBA KIMOJA NDANI YA KANISA MKINGA

 Wanafunzi wa kijiji cha Ronjo Umasaini kata ya Duga Maforoni Wilayani Mkinga Mkoani Tanga wanasomea ndani ya Kanisa kutokana na kijiji hicho kukosa shule.
Mchungaji wa kanisa hilo, Clement amesema wamelazimika kutoa kanisa hilo ili watoto wasikose elimu ambayo itakuja kuwa msaada katika maisha yao ya baadae.
Mwalimu wa darasa Magreth Lishule  amesema wanalazimika kuwasomesha wanafunzi 105 chumba kimoja kuanzia darasa la awali hadi la tatu na wakimaliza ndio ukomo wa elimu yao.
Alisema uwezo wa walimu ambao yeye na mwenzake wamejitolea  wamekuw awakifundisha hadi darasa la tatu na kutokuwa na uwezo wa kufundisha madarasa ya juu.



Mwalimu wa darasa Magreth Lishule akiangalia kazi za mmoja wa wanafunzi wake darasani.

No comments:

Post a Comment