Wednesday, April 19, 2017

WAMASAI KIJIJI CHA RONJO HOROHORO TANGA WAANZA UJENZI KUPISHA SHULE

 Wakazi wa kijiji cha Ronjo kata ya Duga Maforoni Wilayani Mkianga Mkoani Tanga wakianza ujenzi wa jengo kupisha wanafunzi wa watoto hao ambao ni wa jamii ya wafugaji wa  Kimasai kusoma shule. Wafugaji hao wamejikita porini kilometa 30 kutoka Horohoro karibu na mpakani wa Kenya wamekuwa wakiendesha ufugaji ambapo huduma za mahitaji ya kijamii ikiwemo matibabu (Zahanati)  na shule imekuwa kero ya muda mrefu.
Kwa sasa watoto hao wanasoma kwenye kanisa ambapo liko darasa la awali hadi la tatu na baada ya hapo huwa wamekomea kutokana na kutokuwepo kw awalimu wenye uwezo wa kufundisha pamoja na vyumba vya madarasa.
Watoto hao ambao wako 105 na kufundishwa na walimu wawili wa kujitolea na kusemekana walipatiwa mafunzo na Memkwa.




Mzee wa Kimasai Oyaya na Mchungaji wa Kanisa Clement wakipanga matofali huku wakiangaliwa na mama wa kimasai juzi.

No comments:

Post a Comment