Thursday, April 27, 2017

KERO YA MAJI YAZIDI KUWAANDAMA WAKAZI WA MUHEZA, TANGA

 Wakazi wa Mkanyageni Wilayani Muheza Mkoani Tanga wakiwa katika foleni ya maji katika bomba ambalo wamedai huamka usiku wa saa 9 ili kuwahi foleni ambayo haina uhakika wa kupata huduma hiyo muhimu, Kwa muda mrefu wakazi hao wamedai kuwa kero ya maji imewachosha hivyo kuitaka Serikali kuwangalia kwa jicho la huruma.
Akizungumza na tangakumekuchablog, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha Tumbo alisema Serikali iko mbioni kulimaliza tatizo hilo kwa kuanzia kuchimba visima ambavyo vitapunguza adha ya wananchi.
Alisema wakati wa kuyafanya hayo Serikali inatarajia kusambaza maji kutoka Mabayani ambayo itakuwa mwiko wa kero ya maji katika maeneo yote ya Mkanyageni na Muheza kwa ujumla.





 Mkazi wa Mkanyageni ambaye hulazimika kusaka maji mabondeni ambayo sio salama kutokana na kero ya muda mrefu Wilayani humo.





No comments:

Post a Comment