Tanga,
WAJUMBE wa mkutano mkuu
maalumu wa uchaguzi wa Tanga Press Club (TPC) imewachagua viongozi wa nafasi ya
makamo mwenyekiti na katibu msaidizi nafasi ambazo zilikuwa wazi.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Makamo
mwenyekiti, Lulu George, aliwataka waandishi wa habari kujiendeleza kielimu ili
kuifanya taaluma yao kwa weledi.
Alisema waandishi wengi wamekuwa wakibweteka kwa
kiwango walichonacho na kusahau kuwa
taaluma ya uandishi wa habari inakuwa kila siku.
“Nawashukuru kwa kunichagua kwa kura zote bila
kupingwa hata kura moja, hii inaonekana muko na imani name na niwahakikishieni
nitasimamia haki zenu na maendeleo ya umoja wetu” alisema George na kuongeza
“Lakini nikumbushie kitu kimoja ambacho ni
muhimu tuondosheni makundi na kuwa kitu kimoja kila mmoja ajione sawa na
mwenzake” alisema
Kwa upande wake, Katibu msaidizi, Alexsander
Abraham, aliepata kura 14 kati ya 15
alisema anaomba ushirikiano ili kuweza kuienua klabu hiyo.
Alisema atatoa ushirikiano na kuleta umoja na
kuwahakikishia wanachama kuwa atasimamia
haki na maslahi yao ndani ya klabu na katika uandishi wao.
Katibu wa Tanga Press Club (TPC) Anna Makange, akisoma taarifa ya klabu wakati wa mkutano wa marekebisho ya Katiba na kabla ya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya makamo mwenyekiti na Katibu Msaidizi mkutano uliofanyika ukumbi wa klabu hiyo juzi.
Wajumbe wa mkutano wa Marekebisho ya Katiba ya Tanga Press Club (TPC) pamoja na wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Makamo Mwenyekiti na Katibu Msaidizi wa klabu hiyo wakipitia mistari ya Katiba ya Klabu kabla ya kufanyika uchaguzi juzi.
No comments:
Post a Comment