ZULIA LA FAKI
NILIKIONA CHA MTO URITHI WA
BABU 12
ILIPOISHIA
Vile vile nilitaka kujua jinsi yule msichana anavyohusika na mali za babu yangu. Amejuaje kama mali za babu yangu zimepotea?
Au ana maelezo gani ambayo
anataka kunipa kuhusu mali hizo na ameyapata wapi?
Suala la mali lilinipa shauku
lakini suala la mauaji lilinitia
hofu. Ilibidi nigwaye na nifikiri
vya kutosha kabla ya kuamua kwenda huko Mwananyamala.
Baada ya kuwaza kwa muda
mrefu nilitoka pale nyumbani, nikaenda
kwenye mkahawa uliokuwa jirani. Niliagiza chakula nikala huku nikiwaza.
Nilipomaliza kula niliitoka.
Siku ile kulikuwa na mechi kati ya Simba
na Yanga. Nikaenda uwanja wa taifa. Nilikuwa mpenzi wa mpira wa miguu na shabiki wa moja ya timu
hizo.
Niliangalia mpira hadi saa
kumi na mbili jioni. Sikupata furaha kwa vile timu zilitoka sare bila kufungana. Nikarudi nyumbani.
Mpaka muda huo nilikuwa
nimepuuza kwenda Mwananyamala kumuulizia
Sharif Nasri.
Asubuhi ya siku ya pili yake yule
msichana akanipigia simu.
“Mbona hukwenda kule
nilikokuelekeza?” akaniuliza.
“Nitakwenda leo”
“Ni muhimu. Tafadhali
usipuuze”
SASA ENDELEA
Baada ya kunywa chai niliona
niende huko Mwananyamala alikonielekeza huyo msichana ili nikapate taarifa
zake. Nilitarajia si tu ningeweza kugundua msichana huyo alikuwa nani pia ningeweza kujua
sababu ya kuwaua wale watu.
Hata hivyo wakati
nikienda huko Mwananyamala
nilikuwa nikijua fika kwamba yule msichana alikuwa mtu wa hatari.
Lakini kubwa zaidi lililonisukuma
niende, ni vile alivyoniambia kuwa
alikuwa na tarifa ya malli za babu yangu
ambazo mpaka muda ule zilikuwa ni kitendawili nilichoshindwa kukitegua.
Kadhalika mauaji yale ya watu
wanne ambao walikuwa wakidaiwa na babu
yangu yalizidi kunipa shauku ya kutaka kumjua vyema msichana huyo ambaye mpaka muda ule nilikuwa nikiamini kwamba ndiye aliyewaua.
Nilipofika Mwananyamala
niliutafuta mtaa niioelekezwa hadi nikaupata.
Nikaitafuta nyumba yenye namba
aliyonitajia yule msichana. Nilipoiona
nilijisikia kuanza kupata hofu nikajiambia kuwa nami leo naenda kufa.
Sikujua ni kwanini
nilipata hofu. Lakini nilihisi nilipata
hofu kwa sababu nilipagundua mahali ambapo ningepata taarifa za yule msichana
ambazo zilikuwa zikiumiza kichwa changu.
Mbele ya ile nyumba nilikuta
mzee aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha uvivu akivuta mtemba.
Alikuwa mzee mrefu na
mwembamba aliyekuwa na ndevu nyingi nyeupe. Alikuwa amevaa shati jeupe na
suruali nyeupe. Kichwani alikuwa amevaa kofia ya darize.
Jinsi nilivyomsoma kutokana
na mavazi yake na sura yake, alikuwa mswahili wa pwani aliyekuwa amechanganya na
ushirazi. Umri wa mzee huyo haukuwa chini ya miaka sabini na mitano ingawa bado
alionekana kuwa na nguvu za kutosha.
Nilisimamisha gari karibu na
baraza ya nyumba hiyo nikaizima moto na kutoa gea zote na kuvuta hand break na kushuka.
Vile nilivyomuuona mswahili nikamtolea salaam.
“Asalaam alaykum”
“Waalayka salaam”
aliniitikia. Ingawa alikuwa mwembamba,
sauti yake ilikuwa nzito inayokwaruza.
“Habari za hapa?” niliendelea
kumsalimia nikiwa nimesimama mbele yake.
“Nzuri. Karibu” akanikaribisha huku akinitazama kwa macho ya udadisi.
Macho yake yalikuwa
madogo yaliyokuwa na kope nyeupe.
“Samahani mzee wangu,
kulikuwa na mtu ninamuulizia. Aliniambia
ninaweza kumpata hapa”
“Ni nani?”
“Anaitwa Ummy Sharif Nasri”
Mzee nilipomtajia jina hilo alishituka akautoa mtemba wake
midomoni kisha akaniuliza tena huku akiwa amenikazia macho.
“Unasema nani?”
“Ummy Sharif Nasri”
Mzee aliendelea kunikazia
macho.
“Wewe unatokea wapi?”
“Natokea hapa hapa Dar”
“Unamfahamuje Ummy?”
“Sikuwa nikimfahamu tangu
zamani ila jana nilipigiwa simu na msichana
aliyejitambulisha kwa jina hilo akaniambia nikutane naye kwa sababu ana taarifa
za mali za marehemu babu yangu”
“Alikwambia anaitwa Ummy Sharifu Nasri?”
“Ndiyo”
“Alikuelekeza uje kwenye nnyumba
hii?”
“Ndiyo”
“Uliwahi kumuona yeye mwenyewe?”
“Nilimuona jana”
“Una hakika kwamba ulimuona
Ummy?”
“Ndiyo nnilimuonna”
“Nikikuonesha picha yake unaweza kumtambua”
“Ndiyo nitamtambua”
“Hebu subiri”
Mzee alionesha wazi
nilimchanganya akili. Aliinuka kwennye kiti akaingia ndani.
Sikujua ni kwanini alitaharuki. Baada ya muda
kidogo alitoka akiwa ameshika kitabu cha picha.
“Hebu sogea hapa karibu” akanniambia huku akifungua karasa za
kile kitabu.
“Hebu angalia hii picha.
Msichana uliyemuona ndiye huyo?”
Mzee alinionesha picha moja ya ukubwa wa bahasha ya barua. Ilikuwa
ikumuonesha yule msichana akitabasamu.
“Ndiye huyu?” Mzee
akaniuliza.
“Ndiye yeye”
“Mtazame vizuri”
“Nimemtazama vizuri, ndiye
yeye Ummy Sharif Nasri”
“Unaponiambia hivyo unanichanganya…!”
ITAENDELEA kesho Usikose nini kitatokea baada ya picha kuonysha Ummy Sharif Nasri ndio yeye.
No comments:
Post a Comment