Monday, April 10, 2017

ROMA MKATOLIKI AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, AZUNGUMZIA JINSI ALIVYOTEKWA

Roma Mkatoliki akizungumza na vyombo vya habariMsanii Roma Mkatoliki asema anahofia maisha yake siku moja tu baada ya kupatikana katika kituo cha polisi cha Oysterbay.
Akizungumza na vyombo vya habari akiwa na waziri wa mawasiliano Mwakyembe , msanii huyo ameelezea vile walivyotekwa siku ya Jumatano na kufungwa pingu na kitambaa usoni na baadaye kusafirishwa hadi eneo wasilolijua.
Akizungumza na hisia na uchungu mwingi Roma alisema kuwa walipofikishwa walipopelekwa walipata mateso mengi kwa kupigwa hadi siku ya Ijumaa usiku.
Roma Mkatoliki: Tukatolewa tulimokuwepo siku ya ijumaa jioni tuliwa tumefungwa uso, na mikono na miguu. Tukapelekwa sehemu tukatupwa kwenye dimbwi la maji karibu na baharini Roma anasema kuwa alipata fahamu na kuweza kuwafungua wenzake na kutembea mwendo mrefu ambapo
walifika katika maeneo ya ununio.
BBC
Hatahivyo msanii huyo alishindwa kuelezea baadhi ya maswali aliyoulizwa kuhusu mahojiano na waliowateka huku akisema tu kwamba tayari wamewasilisha malalmishi yao kwa polisi kwa ucunguzi.

No comments:

Post a Comment