Tuesday, April 18, 2017

GWIJI LA UIGIZAJI FILAMU MAREKANI AFARIKI

Roger Moore and Clifton JamesMwigizaji Clifton James, aliyeigiza kama Liwali JW Pepper kwenye filamu mbili za James Bond, amefariki dunia akiwa na miaka 96.
Alifariki karibu na mji wake aliokulia wa Gladstone, Oregon, siku ya Jumamosi kutokana na matatizo ya ugonjwa wa kisukari.
James alifahamika sana kutokana na uigizaji wake pamoja na Sir Roger Moore katika filamu za Bonds za Live and Let Die na The Man with the Golden Gun miaka ya sabini.
Binti yake Lynn amesema: ''Alikuwa mtu mpenda watu na mwenye uwazi sana. Alipendwa sana na kila mtu.''
Aliongeza: "Sidhani alikuwa na adui hata mmoja. Kwa kweli tulibarikiwa kuwa na yeye maishani."
BBC

No comments:

Post a Comment