Wednesday, April 5, 2017

KIWANDA CHA SARUJI CHA SIMBA CEMENT YAIPIGA TAFU JUKWAA LA WAHARIRI MILIONI 14



Tanga, KIWANDA Cha Saruji cha Simba Cement Tanga, kimesema moja ya faida yake imekuwa ikiipeleka katika masuala ya kijamii yakiwemo, Afya, Mazingira na Elimu.
Akizungumza mara baada ya Wahariri (Jukwaa la Wahariri TEF)  kumaliza  ziara ya kutembelea kiwanda cha Saruji kujionea shughuli ambazo zinafanywa, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Renhardt Swart, alisema moja ya faida huipeleka kwa wananchi.
Alisema wamekuwa wakisaidia madawati, mifuko ya saruji na majengo pamoja na vyoo kwa shule ambazo zimekuwa zikihitaji msaada.
Akikabidhi shilingi milioni 14 kwa Jukwaa hilo, Swart alisema pesa hizo zinaweza kuwasaidia katika majukumu  yao mbalimbali ukiwemo mkutano mkuu ambao utafanyika kesho Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande wake, Makamo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deudas Balile, alisema amefurahishwa na uzalishaji wa Saruji pamoja na mipango kabambe kiwandani hapo.
Akizungumzia msaada huo, Balile alisema utasaidia katika masuala mbalimbali ya Jukwaa hilo ikiwa na pamoja na  mkutano mkuu wa Moshi kesho na kutoa shukurani na kuwataka wawekezaji wengine kuiga mfano kama huo.




 Makamo Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri wa Habari (TEF), Deudatus Balile (kulia) , akipokea mfano wa hundi wa shilingi milioni 14 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji kiwanda cha Saruji cha Tanga  Simba Cement, Renhardt Swart, kusaidia jukwaa hilo katika majukumu yake ya kila siku ikiwemo mkutano wao mkuu kesho Moshi Mkoani Kilimanjaro.



Afisa Mawasiliano na Masoko kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Tanga , Hellen Maleko, (kulia) akiwakabidhi hundi yenye mfano wa shilingi milioni 14 Wahariri wa Jukwaa la vyombo vya habari mara baada ya kutembelea kiwanda hicho leo ikiwa ni msaada katika mambo yao mbalimbali ukiwemo mkutano wao mkuu kesho Moshi Mkoani Kilimanjaro.



 Eneo la Kware ambalo kiwanda hicho toka kianze uzalishaji wame wamekuwa wakichimba Matirialhadi hii leo ambapo Afisa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Beni Lema amewaambia Wahariri hao kuwa kuna kiwango kikifika watasimamisha uchimbaji na kuanzisha mradi wa Ufugaji Mamba.

Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali ya Habari wakipiga picha eneo la Kware ndani ya Kiwanda cha Saruji Simba Cement  inapochimba Matirial ya kiwanda hicho.

No comments:

Post a Comment