Wednesday, December 31, 2014

ACHOMWA KISU KICHWANI NA KUTEMBEA NACHO HADI HOSPITAL

Huyu amechomwa kisu kichwani, ametembea nacho zaidi ya saa mbili akielekea hospitali

Huyu amechomwa kisu kichwani, ametembea nacho zaidi ya saa mbili akielekea hospitali

KnifeMwanaume mmoja Brazil amewashangaza wengi baada, ameweza kutembea masaa mawili kuelekea hospitali akiwa na kisu kichwani alichochomwa na majambazi waliomvamia akiwa anatoka Club.
Kisu hicho kilizama kichwani kwa urefu wa 30cm kilimpata mwanaume huyo Juacelo Nunes pembeni ya jicho la kushoto na kutokea kwenye shavu wakati akipambana na majambazi hao.
brazilKisu kilipita katika baadhi ya mishipa yake ya damu ambayo ingeweza kumuua kutokana na kuvuja kwa damu nyingi,” alisema daktari Gilberto Albuquerque aliyemhudumia mgonjwa huyo kutoka hospitali ya Teresina alipofikia kupata matibabu.
Kisu hicho kilitolewa na kukabidhiwa Polisi ambao wanaendelea na uchunguzi kuwatafuta wahusika wa tukio hilo.
Daktari amesema mgonjwa huyo kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari na hali yake inaendelea vizuri.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog

No comments:

Post a Comment