Tuesday, December 30, 2014

HIFADHI YA TAIFA YA MKOMAZI YAKABIDHI JENGO LA WODI YA WAZAZI KIJIJI CHA MHEZA SAME


 Wakazi wa kijiji cha Mheza na Maore Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro  wakifuatilia maelekezo ya huduma ya mama na mtoto wakati wa makabidhiano ya mradi wa wodi ya mama na mtoto iliyojengwa na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na kugharimu zaidi ya shilingi miloni 81 ambapo kati yake nguvu za wananchi ni milioni 24.





 Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi akikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa kituo cha wodi ya mama na mtoto kijiji cha Maore Wilayani humo jana kilichojengwa na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kwa gharama zaidi ya shilingi milioni 81 ambapo nguvu za wananchi wamechangia milioni 24. Kulia kwake ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi, Donat Mnyagatwa.

 Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Donat Mnyagatwa akikabidhi taarifa ya mradi wa jengo la wodi ya mama na mtoto kwa Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi kijiji cha Maore Same Wilayani Kilimanjaro jana
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi na wakazi wa kijiji cha Mheza na Maore Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wakifurahia baada ya kuzinduliwa kwa wodi ya mama na mtoto jana kilichojengwa na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kwa gharama zaidi ya shilingi milioni 81 ambapo nguvu za wananchi ni milioni 24

No comments:

Post a Comment