Sunday, December 28, 2014

DUNIA YAUMIZA KICHWA AJALI ZA NDEGE ANGANI

TAARIFA ZA AWALI MWANZO KUHUSU NDEGE YA AIRASIA QZ8501 YAPOTEA IKIWA NA WATU 162 LEO ASUBUHI

Ndege ya AirAsia, QZ8501 iliyokuwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda Singapore iliyopoteza mawasiliano jana asubuhi.Ndugu, jamaa na marafiki wa abiria waliokuwa kwenye ndege ya AirAsia QZ8501 wakiwa na majonzi wakati wakisubiri taarifa kuhusu ndugu zao katika Uwanja wa Ndege wa Surabaya, Indonesia.
Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1 kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.
Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa. Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014 kama ilivyokuwa imepangwa.
Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.
Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito. hapa jamaa na warafikiwa ndugu wakinakili majina ya abiri waliopotea
QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.
Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.
Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta

No comments:

Post a Comment