Wednesday, December 31, 2014

BIBI HARUSI AVURUMISHIWA MAWE AKIWA HOLINI


Hekaheka ya leo December 31 iko hapa, inatoka Vingunguti ambapo Bibi harusi walipigwa mawe katika sherehe

Hekaheka ya leo December 31 iko hapa, inatoka Vingunguti ambapo Bibi harusi walipigwa mawe katika sherehe

Stone II
Hekaheka ya leo December 31 ni ya mwisho kwa mwaka 2014, inatokea Vingunguti Dar es Salaam ambapo watu wasiofahamika wamekuwa na tabia ya kupiga mawe watu waliopo katika sherehe ya harusi ambazo hufanyika kwenye uwanja.
Dada mmoja ambaye jina lake ni Zay amesimulia kuhusu kisa kimoja ambacho kimejitokeza kwenye sherehe ya harusi ambapo Bibi Harusi alipigwa na jiwe jichoni wakati wakiwa katika tukio la kukata keki.
Warushaji wa mawe hawafahamiki na hawakuonekana kwa kuwa walijificha gizani.
Sherehe hiyo ilivunjika baada ya MC wa shughuli naye kupigwa jiwe na kupasuliwa miwani yake aliyokuwa amevaa.

No comments:

Post a Comment