Wednesday, December 31, 2014

MOVE ZINAZONGOZA KWA KUIBWA MWAKA 2014

Movie zilizoongozwa kwa ‘kuibiwa’ kwenye mtandao 2014.

Movie zilizoongozwa kwa ‘kuibiwa’ kwenye mtandao 2014.

the_wolf1
Mwaka 2014 utakuwa mwaka wa kusahaulika kwa Muandaaji filamu Martin Scorsese ambaye filamu yake ya The Wolf Of Wallstreet iliyogizwa na star wa filamu Leornado Di Caprio iliongoza kwa kuibiwa kwenye mtandao kinyume cha sheria .
Vyanzo mbalimbali vya habari nchini Marekani wiki hii vilichapisha orodha ya filamu ambazo zimeongoza kuibiwa kinyume cha sheria yaani ‘Illegal Downloads’ orodha ambayo filamu hii ya Wolf Of Wallstreet iliongoza .
Watumia kompyuta wapata milioni 30 walidownload movie hii kwa kipindi cha kuanzia Januari 1 mpaka desemba 23 huku Movie ya vikaragosi au Animation Film ya Frozen ikishika nafasi ya pili baada ya kuibiwa na watu wapatao milioni 29.9.
Movie iliyoshika nafasi ya tatu klatika orodha ya filamu zilizoshushwa kwa wingi kinyume cha sheria kupitia mtandao wa internet ilikuwa filamu ya RoboCop ambayo ilishushwa mara milioni 29.6 huku Filamu ya Gravity nayo ikiwa kwenye nafasi ya nne baada ya kushushwa mara milioni 29.4
Movie nyingine zilionekana kwenye orodha hii ni “Thor: The Dark World,” “Captain America: The Winter Soldier” na filamu ya  “X-Men: Days of Future Past ambapo zote zilishushwa na watu ambao wanapita idadi ya watu milioni 20 .
12-years-a-slave
Filamu iliyofanya vizuri mwaka huu mpaka kutwaa tuzo ya Oscar huku ikimtambulisha rasmi star toka Afrika Mashariki Lupita Nyong’o ya 12 years a slave ilishushwa kwenye mtandao na watu milioni 23.7  huku American Hustle na Captain Philips nazo zikiingia kwenye roodha hii baada ya watu milioni 23.1 kushusha .

Orodha Kamili .
  1. “The Wolf of Wall Street”: 30.035 millioni
  2. “Frozen”: 29.919 millioni
  3. “RoboCop” (ikiwemo original 1987 movie): 29.879 millioni
  4. “Gravity”: 29.357 millioni
  5. “The Hobbit: The Desolation of Smaug”: 27.627 millioni
  6. “Thor: The Dark World”: 25.749 millioni
  7. “Captain America: The Winter Soldier”: 25.628 millioni
  8. “The Legend of Hercules”: 25.137 milioni
  9. “X-Men: Days of Future Past”: 24.380 milioni
  10. “12 Years a Slave”: 23.653 milioni
  11. “The Hunger Games: Catching Fire”: 23.543 millioni
  12. “American Hustle”: 23.143 milioni
  13. “300: Rise of an Empire”: 23.096 milioni
  14. “Transformers: Age of Extinction”: 21.65 milioni
  15. “Godzilla”: 20.956 milioni
  16. “Noah”: 20.334 milioni
  17. “Divergent”: 20.312 milioni
  18. “Edge of Tomorrow”: 20.299 milioni
  19. “Captain Phillips”: 19.817 milioni
  20. “Lone Survivor”: 19.130 milioni

No comments:

Post a Comment