Monday, December 29, 2014

VILIO, MAJONZI VYAENDELEA INDONESIA, SALA MAOMBI KILA KONA

UPDATES: NDEGE YA AIRASIA QZ8501 ILIYOPOTEA NA WATU 162

Kikosi cha wanamaji nchini Indonesia kikisali kabla ya kuanza zoezi la kuitafuta Ndege ya AirAsia QZ8501 katika bandari ya Pangkal Pinang kwenye kisiwa cha Sumatra.
Kikosi cha wanamaji kikiwa kazini kuitafuta ndege iliyopotea.
Ndugu wa watu waliokuwa kwenye ndege iliyopotea wakifarijiana huku wengine wakilia kwa uchungu.
ZOEZI la kuitafuta Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyopotea ikiwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda Singapore jana limeendelea leo asubuhi.
Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la utafutaji ndege hiyo zinadai kwamba mabaki ya AirAsia QZ8501 yameonekana baharini na kuna uwezekano ndege hiyo ipo chini ya bahari.

No comments:

Post a Comment