Sunday, December 28, 2014

AMUUWA MKE WAKE KWA SHOKA KUMKOSEA KITOWEA CHA KUKU KRISMASS

Mume alikosa kitoweo cha Kuku siku ya Christmas… Kilichofuatia ni ukatili kwa mkewe

Mume alikosa kitoweo cha Kuku siku ya Christmas… Kilichofuatia ni ukatili kwa mkewe

1Kama ulifanikiwa kuisherehekea Christmas ya mwaka huu 2014 kwa amani basi ni heri kwako, kumbe wakati wengine wakisherekea kwa amani Sikukuu hii kubwa ya mwaka kuna sehemu ambazo hakukuwa na heri yoyote siku hiyo.
Story hii ya kusikitisha inatoka Kenya ambapo jamaa mmoja Daniel Imonje, alimpiga mke wake kwa shoka mpaka kufariki, majirani walioshuhudia wakisema eti kisa ilikuwa ni kitendo cha mke wake huyo kutomuandalia mume wake nyama ya kuku siku ya Christmas, badala yake akaandaa rosti ya nyama ya ng’ombe.
Ni wengi waliolaani  kitendo hicho kilichotokea Kijiji cha Shanderema, Kenya na mashuhuda wamesema Daniel alifanya unyama huo akiwa amelewa.
Mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Kakamega baada ya kufanya mauaji hayo kwa ajili ya uchunguzi.
20080626-BackyardChickens
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog

No comments:

Post a Comment