Sunday, December 28, 2014

ATUMIA MBINU MBADALA KUMREJESHA MPENZI WAKE


 Analazimika kutumia mbinu mbadala kumpata mpenzi wa kusafiri naye, wa zamani walimwagana…

Analazimika kutumia mbinu mbadala kumpata mpenzi wa kusafiri naye, wa zamani walimwagana…

couple holding hands (4) (1)Msimu ya sikukuu watu wengi husafiri kwenda maeneo mbalimbali ili kusherehekea pamoja na kutembelea ndugu, jamaa na marafiki,
Jamaa mmoja Canada aliandaa safari kwa ajili yake na mpenzi wake, bonge la vacation kwa kutumia usafiri wa ndege ya kukodi wazunguke maeneo mbalimbali duniani, baadaye mambo yakabadilika baada ya kuzinguana na girlfriend wake, akalazimika kutumia mitandao ya kijamii kutafuta mtu ambaye anafanana jina na mpenzi wake ili tu afanikishe safari hiyo ya kihistoria kwa kuwa ilishindikana kubadilisha jina la mtu ambaye anasafiri naye.
Zali hili ilikuwa ni lazima limuangukie mtu mwenye jina Elizabeth Gallagher, sawasawa na mpenzi wake waliyetengana.
Jamaa huyo Jordan Axani alipata bahati ya kumpata mtu anayefanana jina na mpenzi wake huyo ambaye ni mwanafunzi na safari yao ilitarajiwa kuanza Jumapili ambayo ni leo. 
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kupitia kumekucha blog

No comments:

Post a Comment