Monday, December 29, 2014

MKALI HAILEY BALDWIN BADO HAJATULIA

Ukiitazama hii unadhani bado Justin Bieber na Hailey Baldwin ni marafiki tu?

Ukiitazama hii unadhani bado Justin Bieber na Hailey Baldwin ni marafiki tu?

justtUhusiano ya kimapenzi wa msanii Justin Bieber umeendelea kuchukua nafasi kwenye vyombo mbalimbali vya habari na safari hii tetesi zilizopo ni juu ya uhusiano kati yake na mrembo Hailey Baldwin.
Bieber licha ya kutoweka wazi mapenzi yake na mwanadada huyo huku akisisitiza bado yupo Single baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Selena Gomez, ameonekana akivinjari sehemu mbalimbali za starehe usiku na mrembo huyo katika kipindi hiki cha sikukuu.
bbbbbb
Wawili hao walikua nyumbani kwa Bieber na baadaye kuamua kwenda kupata chakula cha usiku katika moja ya hotel iliyopo New York ambapo walitumia zaidi ya saa moja huku wakionekana kuwa karibu zaidi huku mwanadada huyo akiamua kumzawadia Bieber zawadi.
Baada ya kupata chakula waliamua kwenda kutazama movie ya The Gambler na baadaye kurudi nyumbani kwa Bieber hadi siku ya pili yake asubuhi walipoonekana tena pamoja katika mji wa New Jersey.
lovvvvvBaadaye mchana katika ukurasa wa Twitter Hailey aliweka ujumbe kuwa amefurahi na amekua na usiku wa furaha katika nyumba yake mwenyewe.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog

No comments:

Post a Comment