Thursday, December 25, 2014

MWANA MPOTEVU KUREJEA NYUMBANI

Torres kurudi nyumbani.


Torres kurudi nyumbani.

torres
Klabu za Atletico Madrid na Ac Milan zimeanza mazungumzo juu ya usajili wa mshambuliaji Fernando Torres ambaye kama mambo yatakwenda sawa anaweza kusajiliwa na mabingwa hawa wa ligi kuu ya Hispania ndani ya dirisha dogo la usajili mwezi januari .
Torres ambaye anacheza Ac Milan kwa mkopo akitokea kwenye klabu ya Chelsea amekuwa kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa kuonyesha kiwango bora hali ambayo imemfanya kocha wake Philipo Inzaghi kukata tamaa na mshambuliaji huyo .
Taarifa zaidi zinasema kuwa Milan na Madrid wanaweza kufanya mabadilishano ya wachezaji ambapo Torres ataruhusiwa kujiunga na Madrid huku timu hiyo ikimtoa Alesio Cerci kwenda Milan .
Klabu ya Chelsea imemruhusu Torres kuondoka .
Klabu ya Chelsea imemruhusu Torres kuondoka .
Cerci kwa upande wake ameshindwa kuonyesha ubora wake wa msimu uliopita wakati alipokuwa mfungaji bora wa ligi ya Italia hali iliyowavutia Atletico Madrid kumsajili .
Huko London, England klabu ya Chelsea imetajwa kufikia muafaka na Torres kiasi cha kukubali kumruhusu aondoke bure kwenda mahali kokote ambako atahitaji kwenda na hakuna mpango wowote toka kwa klabu hiyo ya London wa kumzuia .
Fernando Torres alikuwa tishio wakati akiwa liverpool na hajawahi kurudi kwenye kiwango chake tangu aliposajiliwa na Chelsea.
Fernando Torres alikuwa tishio wakati akiwa liverpool na hajawahi kurudi kwenye kiwango chake tangu aliposajiliwa na Chelsea.
Torres amekuwa na wakati mgumu tangu alipoondoka Liverpool mwaka 2011 ambapo hajawahi kurudi kwenye ubora wake uliowahi kumfanya kuwa mshambuliaji tishio barani ulaya.
Fernando Torres anatazamwa kama gwiji na klabu ya Atletico Madrid ambayo aliwahi kuwa nahodha wake baada ya kuichezea tangu akiwa mtoto mdogo na kurejea kwenye klabu hiyo kunaweza kumfanya arudishe upya makali yake .

No comments:

Post a Comment