Saturday, December 27, 2014

KOREA KASKAZINI YAIKOMALIA MAREKANI, YALETA KEBEHI

RAIS OBAMA AITWA TUMBILI NA KOREA KASKAZINI!

Rais Barrack Obama wa marekani amefananishwa na tumbili wa msitu wa TropikiKorea kaskazini na imeilaumu Marekani kutokana na matatizo ya mtandao ambayo yameikumba siku chache zilizopita.
Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananisha rais wa marekani Barack Obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa kwa filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview.

Filamu ya the interview ambayo rasi Obama alishinikizwa ionyeshweFilamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un.
Korea Kaskazini imekana kuhusika kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.

No comments:

Post a Comment