Sunday, December 28, 2014

RONALDO, MZUNGU AU MWARABU, CHEKI HAPA PICHA TOFAUTI

Christiano Ronaldo Akiwa Kwenye Vazi La Kanzu Huko Dubai

Cristiano Ronaldo akiwa kwenye mavazi ya kiislam akipiga picha na mashabiki huko Dubai.
Mchezaji nyota wa mpira wa miguu anaeichezea timu kubwa tajiri duniani Real Madrid alionekana na kupigwa picha na mapaparazi kwenye matembezi yake binafsi Dubai akiwa amevalia mavazi ya Kiislam na yaliompendeza sana.
Cristiano Ronaldo ambaye yeye si Muislam lakini alipendezwa na uvaaji huo kwani alisema aliona watu wengi waishio Dubai ndio vazi lao kuu na kwanini yeye asiwe miongoni mwa waliovaa vazi hilo. Pia hakuwahi kuvaa vazi la dini hiyo alionelea avae kwa ishara ya kuiheshimu dini hiyo na kuona sio kitu kibaya kuwa miongoni kwao kimavazi.
Cristiano Ronaldo akiwa kwenye vazi jingine la kiislamu huko Dubai
Mchezaji huyo alikuwa Dubai wiki iliyopita kwenye mapumziko yake binafsi mbali na shughuli za kimpira. Alienda kutembea huko kabla ya wiki ya sikukuu za christimas. Alionekana ni mwenye kufurahishwa na mandhali ya mji huo pia utamaduni wao wa chakula pia kimavazi ndio mana nae alipendezwa kuvaa kama wao.
Vazi lingine alilovaa mchezaji Cristiano Ronaldo akiwa kwenye matembezi yake binafsi Dubai.
Mchezaji huyo alikaa Dubai kwa siku nne wiki ilopita na baadae aliondoka kurejea Hispania ambapo alijiunga na wachezaji wenzake kwenye kambi ya maandalizi ya mechi zilizoendelea katika ligi ya ichi hiyo amakochezea.

No comments:

Post a Comment