Saturday, December 27, 2014

JE ,SIKU YA LEO NAWE UTAPATA ZAWADI?

Boxing day ya Rapper Ludacris, ni zawadi hii kwa mpenzi wake…


Boxing day ya Rapper Ludacris, ni zawadi hii kwa mpenzi wake…

IMG_0820 Baada ya sikukuu ya Christmas December 25, tumeona mitandaoni watu wakifurahia siku ya jana kwa kupokea zawadi mbalimbali toka kwa wapenzi, ndugu, jamaa na marafiki zao.
Sio Bongo tu kulikuwa na mastory ya kupeana zawadi, kutoka Marekani rapper Ludacris ameona isiwe kesi, nae katoa zawadi kwa mpenziwe.
Boxing day ya 2014 itakuwa historia kwenye maisha ya Ludacris na mpenzi wake Eudoxie Agnan kwa kuwa wapenzi hao walifanya engagement, Eudoxie alivishwa pete ya uchumba baada ya uhusiano wao kuwa hai kwa miaka mingi kama wapenzi wa kawaida.
Ludacris aliwaalika marafiki kadhaa akiwemo Star LeToya Luckett kutoka kundi la Destiny’s Child, na kusafiri nao kutoka Atlanta kuelekea Costa Rica kwa ndege ya kukodi, ndege ilipoanza kupaa Ludacris alimwambia mpenzi wake aangalie dirishani, kulikuwa na maneno yaliyoandikwa Will you marry me?’, Eudoxie hakuwa na neno nje ya kujibu kwa furaha ndiyo‘.
Ludacris alishare picha za tukio hilo katika ukurasa wake wa Instagram na kuandika “She didn’t say yes. She said HELL YES! #milehighproposal”

No comments:

Post a Comment