Thursday, December 25, 2014

VITUKO VYA MASTAA

Unamfahamu mchezaji anayeichukia Krismasi?

Unamfahamu mchezaji anayeichukia Krismasi?

ronnie tweet
Wachezaji wengi wa soka barani ulaya wamekuwa mstari wa mbele kuwatakia mashabiki wao heri ya sikukuu ya krismasi katika kipindi hiki ambacho kila mmoja amekuwa katika mzuka wa sikukuu hii .
Wayne Rooney hakubaki nyuma kwa kutumia mtandao wa twitter kuwatakia mashabiki wake heri ya sikukuu .
Wayne Rooney hakubaki nyuma kwa kutumia mtandao wa twitter kuwatakia mashabiki wake heri ya sikukuu .
Wachezaji hawa kwa kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kama Facebook , Twitter na Instagram wamekuwa wakionyesha ubinadamu wao kwa kutuma ujumbe wa aina mbalimbali wa kuwataka mashabiki wao kuwa na furaha katika kipindi hiki .
Wachezaji wa Juventus ya Italia wakiwatakia mashabiki wao heri ya Christmas.
Wachezaji wa Juventus ya Italia wakiwatakia mashabiki wao heri ya Christmas.
Kwa beki raia wa Ujerumani anayecheza kwenye klabu ya Stoke City Robert Huth hali imekuwa tofauti baada ya mchezaji huyo kuonyesha hisia za kinyume kabisa na wachezaji wengine .
Mchezaji huyu aliustaajabisha ulimwengu kwa kitendo chake cha ku-tweet hisia zake kuhusiana na sikukuu hii ambayo inadhimishwa ulimwenguni kote.
Tweet inayoonyesha hisia za beki Robert Huth kwa sikukuu ya Christmas.
Tweet inayoonyesha hisia za beki Robert Huth kwa sikukuu ya Christmas.
Robert Huth kwa kutumia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter aliandika kuwa anaichukia krismasi na hakutoa sababi za msingi za chuki aliyo nayo kwa sikukuu hii .
Hakuna aliyeweza kufahamu chanzo hasa cha utofauti huu toka kwa beki huyu Mjerumani ambaye amejijengea sifa kama beki mgumu asiyetetereshwa na washambuliaji awapo uwanjani .

No comments:

Post a Comment