Tuesday, December 30, 2014

NICK CANNON ASISISTIZA HATOINGIZA MASHAIRI YA KUMKEBEHI MTALAKA WAKE

Hiki ndicho alichokijibu Nick Cannon kuhusu kuandaa album ya kumponda Mariah Carey…

Hiki ndicho alichokijibu Nick Cannon kuhusu kuandaa album ya kumponda Mariah Carey…

coupleeNick Cannon na mkewe Mariah Carey ni miongoni mwa mastaa waliamua kutengana kwa mwaka huu huku kila mtu akionekana kuendelea na mambo yake.
Licha ya kutengana kwao kuna uvumi kuwa wapo katika kutoelewana,huku Nick Cannon akisema hana sababu ya kutumia mashairi ya albamu yake mpya atakayoitoa wakati wowote kumfikishia ujumbe mke wake huyo kutokana na tofauti zao.
Cannon aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa hajarekodi wimbo wowote wenye lengo la kumchafua Carey “Sitasema kitu chochote kibaya kuhusu Mariah Carey,sisi ni familia iliyotokea kwenye mizizi ya upendo’
totoCannon mwenye miaka 34 na Mariah Carey mwenye miaka 45 walifunga ndoa  yao April 2008 na kufanikiwa kupata watoto wawili lakini baadaye mwaka huu walitengana huku Cannon akiendelea kutoonyesha kumbagua kitu kinachodaiwa ndiyo chanzo cha kutengana kwao.

No comments:

Post a Comment