Sunday, December 28, 2014

PILISI TANGA KUENDESHA MSAKO MAJUMBA YA MADANGURO

Kumekucha blog
Tanga,JESHI la polisi Tanga, limesema litaendesha msako kukomesha biashara ya ngono inayoendeshwa katika majumba ya sterehe pamoja na mitaa inayojulikana kwa kujiuza.
Ujio huo  umekuja baada ya malalamiko ya muda mrefu ya wakaazi wa maeneo ya Centrol na Ngamiani kati kuongezeka kwa biashara ya kujiuza nyakati za usiku jambo ambalo linatishia jamii kumomonyoka kimaadili.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa gazeti hili jana, kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Freisser Kashai, alisema kwa muda mrefu taarifa za kuwepo kwa biashara ya kujiuza wako nayo na hivyo wanajipanga kuikomesha.

Alisema kitendo kibaya zaidi ya kuongezeka kwa biashara ya kujiuza miili ni kuingiliwa na watoto wenye umri mdogo ambao wengi miongoni mwao ni wanafunzi ambao  hutoroka katika mabweni.

“Kwa muda mrefu tumekuwa katika uchunguzi wa jambo hili na tumewakamata wengi lakini tukabaini kuwa ni mtandao mpana----hivyo tukarudi nyuma kujipanga zaidi” alisema Kashai

“Nadhani wewe umekuja wakati muafaka wa suala hili kwani liko jikoni na limeshachemka---tutakavyoanza operesheni ni siri ya polisi ila nikuambie biashara ya kujiuza nitaikomesha” alisema

Alisema polisi iko na taarifa zote za majengo yanayoendesha biashara hiyo na maeneo ya kujiuzia na itanza wakati wowote kuendesha uvamizi mfululizo hadi kukomeshwa ikiwa na pamoja na kuwapeleka mahakamani.

Alisema awali waliweza kuikomesha biashara hiyo lakini baada ya polisi kuacha misako waliweza kurejea tena na kudai kuwa ni kwa kasi hivyo kutaka kurejea kwa nguvu mfululizo na kuikomesha kabisa.

Kwa upande wa usalama wa raia na mali zao, kamanda Kashai, aliwataka wananchi kuelekea mwaka mpya kushirikiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa za matukio na watu ambao watakuwa na mashaka nao.

“Kila mara tumekuwa na utaratibu wa kufanya mikutano na wananchi mitaani kuwaelimisha mashirikiano na polisi kwa kupeana taarifa za kihalifu na usalama---hii imesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza matukio ya kihalifu” alisema Kashai

Alisema utaratibu wa kufanya mikutano na kujumuika na wananchi kumelifanya jeshi hilo kuwa karibu na wananchi pamoja na kurahisisha mawasiliano jambo ambalo limetokomeza matukio ya kihalifu ambayo yalikuwa kikwazo kwa maendeo.

                                       Mwisho

No comments:

Post a Comment