Badala ya michango ya harusi Wachina hufanya mnada huu kila mwaka. >>>
Utamaduni uliozoeleka ni kwamba ukiwa
unataka kuoa ama kuolewa ni muhimu kupitisha ile michango ya harusi kwa
ndugu, jamaa na marafiki ili kufanikisha zoezi hilo. Lakini kwa wenzetu
wa China hali iko tofauti kidogo, wao wana kitu kinaitwa Beijing Size Olympic Wedding Expo.
Beijing Size Olympic Wedding Expo ni mnada unaofanyika mara tatu kila mwaka nchini China
wa vitu vyote vinavyo husiana na harusi, iwe ni magauni, suti, pete,
mapambo, hadi magari ya maarusi unaweza kuvipata kwenye mnada
huo. Dhamira ya mnada huu ni kusaidia kupunguza gharama za matumizi ya
pesa zinazotumika kuaanda sherehe hizo.
Lakini kuna baadhi ya Wachina wanaona
kuwa mnada huu bado ni kitu cha bei kubwa kwao,na vijana wengi wa
Kichina sasa hivi wameamua kuanzisha style mpya ya kufunga harusi
zinazoitwa Do-It-Yourself Wedding! Aina hizi za harusi hufanyika majumbani na ndugu, jamaa na marafiki.
Harusi za namna hii hazihitaji mialiko
kwani mialiko hutolewa kwa njia ya tangazo la bango kwenda kwa ndugu
jamaa na marafiki, na MC anaweza kuwa mtu yoyote aliealikwa. Chakula
kinapikwa na wanafamilia na suala la vinywaji linasimamiwa na marafiki.
Nimekusogezea baadhi ya picha za mnada huo pamoja na baadhi ya picha za aina hii ya Do-It-Yourself Wedding.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment