Saturday, July 18, 2015

HADITHI SEHEMU YA (7)

HADITHI hii inaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha cha Tiba Asilia (Mkombozi Sanitarium Clinic) Mabingwa wa kutibu magonjwa sugu yaliyoshindikana. Mkombozi wako na mashine kubwa za kisasa za kupima mwili mzima. Kituo kiko na madaktari waliobobea katika kutibu magonjwa hata yaliyoshindikana. Mkombozi wapo Tanga mkabala na Raha Leo Chuda. Wasiliana nao kwa simu 0654 361333
 

 
ILIPOISHIA
 
Nikadhani labda ni kweli atajifungua mapacha. Mimba ilipotimiza miezi mitatu Halima aliota akifanya tendo la ndoa na mwendawazimu. Alipoamka akaanza kuumwa tumbo!
 
“Una nini?” nikamuuliza nilipomuona akifurukuta.
 
Akanihadithia ile ndoto aliyoota kasha akaniambia alipoamka aliona tumbo linamuuma.
 
Wakati ananieleza hali ilizidi kuwa mbaya. Nikafikiria nimpeleke hospitali lakini ile mamba ikatoka muda ule ule.
 
Sikujua alikuwa amepatwa na tatizo gani. Ilikuwa saa kumi na mbili asubuhi. Nikatoka naye na kumpakia kwenye teksi, tukaenda hospitali ya Bombo.
 
Tulipofika hospitali nilimpigia simu rafiki yangu Dk Augostino Kweka. Kwa bahati njema alikuwa pale pale hospitali, akaja kumtazama mke wangu kisha  akaniambia.
 
“Anahitaji kusafishwa. Mimba haikutoka yote”
 
Dk Kweka alinisaidia sana. Alilichukua jukumu lile kirafiki. Mpaka inafika saa tatu mke wangu alikuwa ameshasafishwa.na kupelekwa wodini. Mimi mwenyewe nilikuwa hapo hapo hospitali muda wote.
 
SASA ENDELEA
 
Baada ya kupelekwa wodini Dk Kweka aliniita, nikaenda wodini na kumuona mke wangu. Hali aliyokuwa nayo wakati anapelekwa kufanyiwa usafishwaji, siyo aliyokuwa nayo wakati ametolewa. Alikuwa na afadhali sana.
 
Nikamshukuru Dk Kweka nay eye akanishukuru pia.
 
“Unaweza kurudi naye nyumbani” akaniambia.
 
“Tatizo lake limekwisha kabisa?” nikamuuliza.
 
“Limekwisha isipokuwa kila wiki umlete kuangalia maendeleo yake”
 
“Lilikuwa ni tatizo gani?”
 
“Mimba ilikuwa haikushika sawa sawa. Ana udhaifu kwenye kizazi chake. Katika hali kama hiyo anapopata mshituko, hofu au fadhaa, mara moja mimba inaweza kutoka”
 
Nikahisi ile ndoto aliyoota ndiyo iliyomshitua na kusababisha mimba hiyo kuporomoka.
 
“Asante dokta, sasa unatushauri nini?”
 
“Kama nilivyokwambia kila wiki mlete hapa hospitali, nione maendeleo yake”
 
“Sawa dokta, nitafanya hivyo”
 
Baada ya hapo niliondoka na mke wangu tukarudi nyumbani. Kila wiki nikawa nampeleka hospitali kufanyiwa uchunguzi na Dk Kweka. Wiki nyingine ambazo sikuwa na nafasi alikuwa akienda mwenyewe.
 
Zoezi hilo lilichukua wiki sita ndipo tukaacha kwenda hospitali. Dk Kweka akanihakikishia kuwa tatizo la mke wangu halikuwepo tena.
 
“Kama unataka mimba nyingine kazi kwako” Dk Kweka akaniambia kwa utani.
 
“Asante sana. Kwa kweli ninakushukuru kwa msaada wako” nikamwambia.
 
Siku moja ambayo sitaisahau maishani mwangu nilikuwa kwenye kiwanja cha ndege cha Tanga. Kulikuwa na ndege ya abiria iliyotua kutoka Zanzibar.
 
Nikapata abiria mmoja ambaye alivutia sana hisia zangu. Alikuwa ni kijana ambaye nilisoma naye katika shule ya sekondari ya Usagara. Mimi nilikomea kidato cha nne, yeye alifanikiwa kuendelea kidato cha tano na cha sita. Alikuwa anaitwa Zacharia.
 
Tangu tulipoondoka shule hatukukutana tena hadi siku ile. Miaka minane ilikuwa imeshapita. Mbali ya kufurahi kumuona pia alinishitua, kwanza kumuona akishuka kwenye ndege na kwa jinsi alivyokuwa amevaa na kupendeza.
 
Alikuwa amevaa suti nyeusi. Koti lake alikuwa amelivua na kulipachika begani. Ndani ya suti kulikuwa na shati jeupe na tai yangi nyekundu. Uso wake uliokuwa umenawiri ulionesha mwenzangu alitoka kwenye neema
 
Kukutana kwangu na Zacharia baada ya kufarakana kwa karibu miaka minane kulikuwa ndio mwanzo wa masahibu niliyokutana nayo amabayo sitayasahau kamwe.
 
“Oh Machawi! Habari za siku?’ Hivyo ndivyo Zacharia alivyonisalimia huku akinipa mkono mara tu aliponiona ndani ya jengo la kiwanja cha ndege.
 
Machawi lilikuwa jina langu la utani ambalo vijana wenzangu walikuwa wakiniita shuleni. Walianza kuniita mchawi kwa sababu nilikuwa na tabia ya kutoroka toroka shule. Naweza kuonekana msitarini lakini wanafunzi wakiingia darasani hawanioni! Nimeshatoroka. Nikaitwa mchawi. Baadaye jina hilo likabadilika likawa Machawi.
 
“Nzuri Zacharia. Kumbe unaishi Zanzibar?”
 
“Nilienda kwa muda, niko Dar”
 
“Kikazi uko wapi?”
 
“Baada ya kuchukua shahada yangu ya sheria niliajiriwa na Wizara ya mambo ya nje”
 
“Nimefurahi kukuona, karibu tena Tanga”
 
“Asante. Nahitaji teksi ya kunipeleka mjini”
 
“Mimi pia ni dereva wa teksi. Hapa nimefuata abiria”
 
“Kumbe unaendesha teksi! Vizuri sana. Basi twenzetu”
 
Nikatoka naye. Mara tu baada ya kujipakia kwenye teksi mazungumzo yakaanza.
 
“Ajira zimekuwa ngumu sana. Nimeangukia kwenye udereva” nilimwambia Zacharia wakati nikiiwasha teksi.
 
ITAENDELEA KESHO na usikose uhondo huu nini kitatokea

No comments:

Post a Comment