Tangakumekuchablog
Tanga, IMAMU
Mkuu wa Msikiti wa Ibadhi Tanga, Sheikh Mohammed Said, ameitaka jamii kuelekea
Uchaguzi Mkuu kudumisha amani na utulivu uliopo na kuacha kushabikia vyama vya
siasa na kupelekea kuhamasiana.
Akihutubia Swala ya Idd El Fitri
jana, Sheikh huyo alisema ni wajibu wa kila mtu kutambua kuwa amani iliyopo
ikitoweka ni vigumu kuirejesha na hivyo
kila mmoja kuhakikisha anatambua wajibu wake.
Alisema vipindi vya chaguzi hutokea
jamii kuhamasiana kwa mambo ya kisiasa jambo ambalo amedai kuwa ni baya na
halifai kutokea na hivyo kuitaka kutambua amani iliyopo na kila mmoja kuwa
mlinzi wa mwenzake.
“Ndugu zangu waislamu leo
tumekusanyika hapa tukiwa kitu kimoja ndugu moja na hakuna mbora kwa mwenzake----hadhara
hii iwe kichocheo cha umoja wetu kwa kupendana na kuhurumiana” alisema Mohammed
Sheikh huyo aliitaka jamii kupendana
na kuhurumiana na kuwa na ada ya kusameheana kwa kila jambo na kudai kuwa
kufanya hivyo kutapelekea kupata rehma za Allah.
Alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa
hawasemeshani wala hawatembeleani jambo ambalo amesema ni baya kwa Mwenyezi
Mungu na hivyo kuwatAka kuitumia siku hiyo kwa kusameheana.
Akizungumzia kuhusu kuwasaidia
yatima na wasiokuwa na uwezo, Sheikh Mohammed aliwataka wenye uwezo kuwapatia
misaada na kuweza kujikimu na maisha kama wengine .
Alisema kufanya hivyo kutaiwezesha
jamii hiyo kuishi maisha mazuri kama wengine
na kuacha kunung’unika kukosa huduma muhimu za kujikimu.
Alisema
watu wasiokuwa na uwezo wamekuwa wakipata shida nyingi zikiwemo za
matibabu na elimu hivyo ni wajibu watu wenye uwezo kuziangalia jamii
hizo.
Waislamu wakinunua nyama soko kuu la Ngamiani Tanga ikiwa ni kusherehekea Sikukuu ya Idd El Fitri iliyosherehekewa na Waislamu kote Ulimwenguni jana.
No comments:
Post a Comment