Tangakumekuchablog
Tanga,MBUNGE wa
jimbo la Tanga mjini, Omar Nundu,(CCM) amewataka viongozi wa kata ya Pongwe na
watendaji wa kijiji cha Kisimatui,kuitumia mifuko ya saruji iliyopewa na
kiwanda cha saruji cha Simba Cement kuitumia kwa malengo iliyokusudiwa.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi
wa kituo cha Afya kinachojengwa kwa nguvu za wananchi jana, Nundu aliwataka
viongozi na wananchi kuitumia saruji hiyo kwa malengo iliyowekwa na kumaliza
kero ya kufuata matibabu masafa marefu.
Alisema ujio wa msaada wa mifuko 300
ya saruji ni ishara njema ya wakazi wa kijiji cha Kisimatui na vijiji vya
jirani kumaliza kero ya matibabu na hivyo kuwataka saruji hiyo itumike kama iliyokusudiwa.
“Nawaomba saruji hii itumike kwa
matumizi yaliyokusudiwa na ninyi viongozi wa kata na kijiji kuhakikisha kasi
muliyoianza iwe endelevu----najua kutakuwa na changamoto nyingi ila ndio
kuelekea kuliko na mafanikio” alisema Nundu
Kwa upande wake Diwani kata ya Pongwe Uzia, aliwataka
wananchi wa kijiji hicho cha Kisimatui, kuwa na moyo mmoja na kufanya harambee
ya michango pamoja na vijana kujitolea upigaji wa matofali na uchotaji wa maji.
Alisema kufanya hivyo kutawezesha jengo
hilo kumaliza mapema na kulikabidhi kwa halmashauri ya jiji kuanza kwa huduma
jambo ambalo litakuwa msaada kwa wajawazito wazee na watoto.
“Kwa pamoja jamani wake kwa waume
tuwe na moyo mmoja wa kulimaliza jengo letu anawezesha kuleta nondo na
maji----kila mwenye nguvu zake azitoe kwa nia moja” alisema Uzia
Alisema kukamilika kwa jengo hilo
kutawawezesha wakazi wa kijiji cha Kisimatui na vya jirani kumaliza kero ya
kufuata matibabu na hivyo kuitumia fursa zzilizoko mble yao kwa kutoa ili lengo
liweze kukamilka.
Mbunge wa jimbo la Tanga mjini, Omar Nundu akiangalia
msingi wa jingo la kituo cha Zahanati kijiji cha Kisimatui kata ya Pongwe .
Mbunge wa jimbo la Tanga, Omar Nundu (CCM) (katikati) akikabidhiwa mifuko ya saruji iliyotolewa na kiwanda cha saruji cha Simba Cement jana kijiji cha Kisimatui kata ya Pongwe na Diwani wa kata hiyo Uzia Juma (kushoto) kulia ni Afisa mtendaji kata, Salim Mdoe.
No comments:
Post a Comment