50 Cent kwenye headlines, ajikuta matatani mahakamani, atangaza kufilisika!
Kumekuwa na stori nyingi kuhusiana na rappa 50 Cent kutoka Marekani, moja kubwa kuhusu yeye ilikuwa ni stori inayohusiana na yeye kuvijisha sex tape ya mwanadada Lastonia Leviston ili kumuaibisha mshindani wake Rick Ross.
Kesi ikaenda Mahakamani na 50 Cent anatakiwa alipe fine ya dola Mil.5 sawa na Billioni 10 za Kitanzania kwa mwandada huyo.
Headlines za 50 Cent
leo ziko tofauti, mwanasheria wa rappa huyo ametangaza kufilisika kwa
msanii huyo baada ya kuwasilisha Mahakamani document zinazoonyesha kuwa 50 Cent ana madeni yasiopungua dola Mil.50 sawa na Bil.100 za Kitanzania.
Kutokana na mujibu wa Sheria iitwayo Chapter 11,
mtu anaruhusiwa kupeleka mahakamani documents na vielelezo vingine
vinavyotoa nafasi makampuni kujilinda na kuokoa baadhi ya biashara
zake wakiwa wanakabiriana na madeni makubwa.
Msemaji wa mwanasheria wa 50 Cent , Travis Carter
amesema msanii huyo amelazimika kufanya hivyo kuweka mambo yake ya
kiuchumi sawa lakini hii haimanishi rappa huyo hana uwezo wa kusimamia
biashara ama pesa zake.
Kwenye Interview moja 50 Cent alisema: “Kufanya
hivi kuna nilinda mimi na maslahi yangu ya biashara nyingi
ninazojihusisha nazo, ni kawaida kwa wafanya biashara kufanya hivi ni
sawa na kulinda mifuko yangu. Uwezo ninao sema narekebisha tu vitu fulani
kwa faida yangu na wadeni wangu”.
Kwenye mahujiano na waandishi wa habari Travis Carter alisema: “Maslahi
yake ya kibiashara yataendelea kama kawaida na ataendelea kujihusihsa
na biashara zake zingine na kuendelea kufanya kazi kama entertainer”.
Kwa sasa rappa 50 Cent anaishi Connecticut Estate kwenye nyumba alioinunua kutoka kwa boxer Mike Tyson mwaka 2003.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment