Tangakumekuchablog
Muheza, MDAU wa
maendeleo ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Muheza Mkoani Tanga, Omary Mhando maarufu (walawala) amesema endapo atateuliwa kuwa Mbunge
atahakikisha kero ya maji Wilayani humo inafikia kikomo.
Omary maarufu kwa jila la walawala
alichukua fomu jana ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge
jimbo la Muheza na kueleza vipaumbele vyake na kusema jambo la kwanza ni
kulimaliza tatizo la maji na soko la machungwa.
Alisema kwa miaka mingi wakazi wa
Muheza wamekuwa katika shida ya kupata maji na badala yake wanatumia maji ambayo
sio salama na hivyo kuwataka wakazi wa jimbo la Muheza kumuunga mkono ili kuwa Mbunge wao.
“Kipaumbele changu cha kwanza ni
kuhakikisha kero ya maji ninaipatia ufumbuzi wa haraka-----hakuna sababu sisi
kukosa maji wakati vyanzo vingi vipo ikiwemo milima na mito” alisema Walawala
na kuongeza
“Niwaahidi wananchi wa jimbo hili
kuwa nimejitolea kuwahudumia kwa nguvu zangu zote----sehemu ya mapato katika
biashara zangu nitayaingiza kusukuma maendeleo” alisema
Akizungumzia kilimo cha machungwa
Wilayani humo, Walawala alisema hakuna sababu ya mkulima wa zao hilo kuwa
masikini kwa humnufaisha mtu wa nje na hivyo kusema atazungumza na wawekezaji
wa ndani na nje kujenga kiwanda cha kusindika matunda na uwepo wa soko la uhakika.
Alisema kwa miaka mingi mkulima wa
Muheza ni mlalahoi hana mabadiliko katika kilimo chake na wakati wa mavuno
wamekuwa wakilanguliwa na kuwatajirisha wageni kwa kuuza kwa bei ya kutupa.
“Muheza imejaliwa kuwa na rutba
nzuri kwa kilimo cha mahindi miwa na machungwa----iweje leo mkulima huyo
anazidi kuwa masikini na kufanywa mtaji kwa matajiri” alisema Walawala
Alisema endapo atakuwa Mbunge
atajenga kituo cha kupokea na kutoa habari za kilimo kikiwa na lengo kupeana
taarifa za matukio ya kilimo yakiwemo ya kutokomeza wadudu waharibifu akiwemo
Nzi wa machungwa.
Kada Maarufu wa CCM Wilayani Muheza Mkoani Tanga, Omary Mhando maarufu (Walawala) (kulia) akikabidhiwa fomu ya Ubunge na Katibu Msaidizi CCM Wilaya ya Muheza, Tija Magoma jana.
No comments:
Post a Comment