Saturday, July 4, 2015

SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO, JUNE04 TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi sita na wanaojiendeleza kielimu. Kituo kiko na walimu waliobobea katika masomo. Pia kituo kiko na Hosteli. Pia wanatoa kozi ya Kiiingereza na Computer na kutoa Chati. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 7727246

In Case
MWANANCHI
Wakati vikao vya juu vya CCM vikikaribia kuanza mchakato wa kumpata mgombea Urais wa chama hicho, mji wa Dodoma umeanza kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali.
Uchunguzi uliofanywa na Gazeti la Mwananchi kwenye maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma hadi jana, umebaini kuwa tayari nyumba nyingi za kulala wageni na hoteli zimeshajaa.
Baadhi ya wajumbe wa vikao hivyo ni wabunge ambao tayari wako Dodoma wakiendelea na Bunge, wengine ni wapambe wa makada waliokuja kurejesha fomu za kuwania Urais ambao hawajaondoka.
Baadhi ya Mameneja wa hoteli hizo walisema watu hao wataondolewa kuanzia Julai 6 iwapo hawatakuwa miongoni mwa waliopangiwa vyumba, huku kukionekana pia baadhi ya wenyeji wameanza kukarabati nyumba zao kwa ajili ya kupangisha wageni mbalimbali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime amewahakikishia wageni kuwa Jeshi lake limejiandaa vizuri kwa ugeni huo mkubwa utakapoingia, kuishi na hadi kuondoka.
MWANANCHI
Hali tete ndani ya Ukumbi wa Bunge jana iliendelea kutanda wakati Spika Anne Makinda alipolazimika kuahirisha kikao asubuhi kutokana na kelele na baadaye Wabunge saba wa upinzani kuadhibiwa, wakiwamo watano waliozuiwa kuhudhuria hadi kumalizika kwa Bunge la 10.
Hali hiyo ndani ya Bunge iliendelea kwa siku ya pili mfululizo na mara zote kusababisha Spika kuahirisha vikao baada ya shughuli za Bunge kushindwa kuendelea kutokana na kelele za wapinzani wanaopinga kitendo cha kuwasilishwa miswada mitatu kwa hati ya dharura wakidai hakuna haja ya haraka hiyo.
Jana Spika Makinda aliibuka na dawa mpya na kuitumia Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwaadhibu wabunge hao saba.
Wabunge John Mnyika, Moses Machali, Tundu Lissu, Felix Mkosamali na Paulin Gekul wamefungiwa kushiriki vikao kuanzia leo hadi Bunge litakapovunjwa Julai 9.
Wabunge wengine wawili, Mchungaji Peter Msigwa na Rajab Mbarouk wamefungiwa kushiriki vikao viwili kuanzia leo baada ya Kamati hiyo kuwatia hatiani wawakilishi hao wote saba kwa kudharau mamlaka ya Spika.
Wengine watatu, Joseph Selasini, Khalifa Suleiman Khalifa na Rajabu Abdalah walitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo leo saa 4:00 baada ya wito wa kuwataka wahudhurie jana kuchelewa.
Mashtaka yetu yaliendeshwa kwa haraka, hatukupatiwa muda wa kutosha kujieleza wala kumtumia wakili,” alisema Machali baada ya Bunge kuahirishwa.
Mbunge Tundu Lissu alisema ni bora kufukuzwa kuliko kuendelea kushuhudia gesi ya Watanzania ikiuzwa kwa nguvu bila ya huruma… Mchungaji Msigwa alisema hata angefungiwa kushiriki vikao vyote, asingeathirika.
Kila siku asubuhi na mapema tangakumekuchablog inakupa kurasa mwanzo mwisho za magazeti yanayochapishwa nchini  na kukupa uchambuzi wa habari kubwa  zilizopewa uzito magazetini, kila kitu ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment