Ndege kubwa zaidi duniani yatua Australia


Maelfu ya watu
nchini Australia walikusanyika kutizama ndege kubwa
zaidi duniani ya Antonov An-225 Mriya, ilipowasili mjini Perth nchini
humo.Misongamano ya magari ilifunga barabara wakati umati ulikusanyika kutizama kuwasili kwa ndege hiyo.
Ndege hiyo ilitoka mjini Prague na kusimama maeneo kadha mashariki ya kati na Asia, ikiwa safarini kwenda Australia.
Ndege ambayo ndio kubwa zaidi duniani inadaiwa kama ingefanya safari ya kuja Tanzania basi hakuna uwanja ambao ingeweza kutua.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment