Tangakumekuchablog
Tanga, POLISI
Mkoani Tanga imekamata shehena ya madawa ya kulevya aina ya mirungi inayodaiwa
kufika tani mbili iliyofichwa katika
uvungu wa basi la abiria la Smart Bus kijiji cha Mtibwani Wilayani Mkinga
ikisafirishwa kuelekea Dar es Salaam.
Tukio hilo kubwa kufichuliwa limezusha taharuki kwa
wananchi na kudaiwa kuwa wasafirishaji wa madawa ya kulevya wamekuwa wakitumia
mbinu mbalimbali na kuwapiga chenga polisi.
Jiji la Tanga limekuwa katika
taharuki kufuatia matukio ya ujambazi kuvamia maduka makubwa na vituo vya
mafuta kisha kupora pesa pamoja na kuuwa raia jambo ambalo jeshi hilo limekuwa
likipeleka nguvu zake nyingi katika ulinzi na usalama.
Katika kuhakikisha linatokomeza
matukio ya Ujambazi na upitishaji wa madawa ya kulevya Polisi imekuwa ikifanya
upekuzi katika majengo zikiwemo hoteli na msako katika mapango ya Amboni.
Katika misako hiyo Polisi kwa
kushirikiana na vyombo vya usalama
imefanikiwa kukamata vifaa mbalimbali vilivyokuwa vitumiwa na majambazi
zikiwemo magobore, mapanga , nguo za kiejshi na risasi 30..
Akizungumza na vyombo vya habari mapema
jana, Kamanda wa Polisi Tanga, Leornard Poul ametangaza kiama kwa wasafirishaji
wa mihadarati ya madawa ya kulevya na kusema kuwa yoyote ambaye atagundulika
kusafirisha au kuuza atapelekwa mahakamani moja kwa moja.
Alisema polisi wakati ikilifanyia
upekuzi gari hilo iligundua shimo kubwa lililozibwa kwa bati ambalo ni
vigumu kugundua na kukuta shehena kubwa
ya miringi iliyowekwa katika viroba vya plastiki.
“Tulipokea taarifa kutoka kwa raia
wema kusafirishwa kwa mirungi ikiwa imefichwa katika muti maalumu ambalo ni
vigumu kuelewa na kudhani ni chesesi ya gari” alisema Paul na kuongeza
“Wakati wa upekuzi polisi ilitilia
mashaka moja kati ya uvungu wa basin a kukuta moja ya mabati yakiwa yamefungwa
kwa tibiti ambazo hufungwa na kufunguliwa bila kugundua” alisema
Alisema kwa sasa polisi kwa kushirikiana
na polisi jamii imekuwa ikifanya upekuzi kila gari pamoja na kufanya doria
katika njia za panya ambazo imegundulika mirungi huwekwa katika magunia ya mkaa
na kusafirishwa kwa pikipiki na baskeli.
Kamanda Poul alisema kwa sasa polisi
inawashikilia mmiliki wa Basi la Smart , Nuru Mzee (44) na dereva wake, Salim
Ali (28) kwa uchunguzi na mara baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa
basi hilo, dereva wa Basi hilo, Salim Ali, alisema anashangaa kuona anajumuishwa
katika tuhuma ambazo amedai kuwa hajui lolote zaidi ya kuendesha gari na
kuangalia usalama wa abiria.
Alisema hahusiki na usafirishaji wa
mirungi hiyo na kusema sio kazi yake ya kukagua mizigo na kuhoji hivyo kutaka
uchunguzi ufanywe kwa kina kwa madai wajibu wake ni kuendesha gari tu.
“Mimi kazi yangu ni kuendesha gari
kuhakikisha abiria wangu nawasafirisha salama na kuwafikisha mwisho wa safari
yao, suala la mizigo sihusiki na sijui lolote mie” alisema Ali
Alisema ameshtusha kuona kuna
shehena hiyo ya mirungi kwenye gari ambayo amepewa siku 15 zilizopita na hivyo
kusema hajui lolote ila kwa vile jambo liko polisi anaiwachia ifanye kazi yake.
Mwisho
Kamanda wa polisi Tanga, Leornard Poul, akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya kilo ya mirungi kati ya kilo 802 iliyokamatwa katika kizuizi cha polisi Mtimbwani barabara ya Tanga, Horohoro iliyokuwa imefichwa katika uvungu wa basi la kampuni ya Smart
Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Leornard Poul, akiwaonyesha waandishi wa habari mbinu iliyokuwa ikitumiwa na wasafirishaji wa mirungi katika basi la kampuni ya Smart katika kizuizi cha polisi cha Mtimbwani Barbara ya Tanga, Horohoro juzi. Shehena ya hiyo mirungi ilikuwa imefichwa katika moja ya uvungu wa gari na kuzibwa bila kugundua kwa urahisi.
Basi la Kampuni ya Smart Bus likiwa nje ya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Tanga na kuonyeshwa na waandishi wa habari kama wanavyoonekana wakiwa wakifanya mazungumzo na dereva wa basi hilo Salim Ally.
No comments:
Post a Comment