Iko hapa tayari U Heard ya leo Desemba 9, Bendi ya Skylight imehusika.
Baada ya Soudy kumtafuta Meneja wa Skylight Band
Aneth Kushaba amesema ni kweli walitishiwa bastola na Promota ambaye
aliwatapeli hela baada ya kufanya naye makubaliano ya kufanya naye show
kwa makubaliano kulipwa hela siku moja kabla ya show kama mkataba
unavyosema lakini promota huyo hakutimiza.
Siku ya show walikubaliana kwamba
Skylight wapate mtu mmoja ambaye atakuwa akipokea kiingilio lakini
baadaye waliamua kumfuata promota huyo ili awaongezee pesa za malipo ya
show hiyo lakini aligoma kuwapatia malipo hayo na kumtishia kumpiga
risasi Meneja huyo wa Skylight huku akimtukana.
No comments:
Post a Comment