Fuatilia hadithi hii ya kusisimua kila siku na usikose
KISIWA CHA HARISHI (3)
Tulitoka katika kile chumba
tukaingia katika chumba kingine. Pia tulikuta kitanda na makabati. Tukawa tunatazamana
kwa mshangao. Kutoka hapo tulichangukana. Kila mmoja akawa anafungua chumba
alichotaka na kuangalia ndani.
Mimi niliingia katika vyumba
viwili. Nilipoingia chumba cha tatu nilishituka nilipomuona msichana mzuri
amelala kitandani. Alikuwa amelala usingizi kabisa huku amejifinika shuka
kuanzia miguuni hadi shingoni. Uso wake uliokuwa wazi ulikuwa umeelekea upande
wangu.
Nilipomuona nilisita kwenye
mlango na kujiuliza msichana huyo ni nani na kwanini alikuwa peke yake katika
jumba hilo.
Baada ya kusita kidogo
niliingia ndani. Nilikuwa nataka kuhakikisha kama
alikuwa hai kweli au amekufa.
Nilipofika karibu yake,
msichana huyo alifumbua macho ghafla. Akashituka aliponiona.
“Wewe nani?” akaniuliza kwa
mshangao akitumia lugha ya kingazija ambayo nilikuwa siijui vizuri. Lakini
nilimjibu kwa Kiswahili.
“Mimi ni mgeni katika kisiwa
hiki na katika jumba hili, je wewe ni nani?”
Alikuwa anajua Kiswahili.
Akanijibu kwa Kiswahili cha kipemba.
“Miye ni Yasmin, binti wa
Rais Shariff Abdilatif wa Comoro!”
SASA ENDELEA
Nilishituka sana aliponiambia yeye ni binti wa Sharif
Abdulatif wa Comoro.
Papo hapo nikakumbuka ile
harusi iliyovunjika kati ya binti wa rais wa Comoro na mwana wa mkuu wa majeshi
ya ulinzi nchini humo.
Mimi nilikuwa mmoja wa
waalikwa kutoka Zanzibar
na nikashuhudia maajabu. Yasmin alitoweka katika mazingira ya kutatanisha baada
ya gari iliyokuwa inampeleka hospitali kupasuka tairi na kuingia kwenyenye
mtaro. Yasmin alikuwa anakimbizwa hospitali baada ya kuanguka ghafla wakati
baba yake Rais Sharif Abdulatif anataka kutoa idhini ya kumuozesha binti yake.
Baada ya kutoweka ghafla
kwenye gari, Yasmin hakupatikana tena na sasa mwaka ulikuwa umeshapita.
Ingawa sikuwahi kuonana naye
uso kwa uso lakini niliona picha zake katika magazeti na televisheni wakati
habari zake zilipokuwa zinaandikwa na kutangazwa.
Alikuwa ndiye Yasmin kweli
binti wa Rais Sharif Abdulatif wa Comoro.
Kwa kweli tukio la kumkuta
ndani ya jumba hilo
na katika kisiwa kile kisicho na watu, mbali ya kunishitua, liliniongezea hofu
mara dufu.
“Wewe ni binti wa Rais wa
Comoro” nikamuuliza kwa mshangao.
Huku akinyanyuka kwenye
kitanda na kuketi msichana huyo alinijibu.
“Ndiye mimi. Rais Sharif
Abdulatif ni baba yangu”
Nikiwa kwenye mshangao
niliendelea kumtazama msichana huyo bila kummaliza. Alikuwa amevaa shumizi
inayoonya. Alipoketi alijifunga ile shuka kwenye mwili wake kama
mtu aliyekuwa anaona baridi. Lakini nilijua alikuwa anajisitiri kwa sababu
sumizi aliyovaa ilikuwa inaonya.
Kwa tamaduni za kiislamu na
za kule Comoro mwanamke hatakiwi kuonekana mwili wake pamoja na kichwa chake.
Lakini Yasmin kwa sababu ya
kutaharuki alisahau kujifinika kichwa. Nywele zake za mawimbi zilizokuwa ndefu
zilikuwa zimeshuka na kumfikia mabegani.
“Yasmin umefikaje huku?”
nikamuuliza.
Yasmin akanitazama. Macho
yake makubwa yenye mboni za rangi ya kahawia yalinifanya nikiri kimoyomoyo kuwa
Yasmin alikuwa mzuri.
Badala ya Yasmin kunijibu, na
yeye akaniuliza.
“Kwani wewe umefikaje hapa?”
“Mimi siko peke yangu, nina
wenzangu na tumefika hapa kwa bahati mbaya. Sisi ni wavuvi kutoka Zanzibar. Chombo chetu
kilipigwa na dharuba kikapata hitilafu. Kwa siku nne kilikuwa kinaelea kwenye
maji, hatujui tunakokwenda. Leo siku ya tano ndio tumetokea kwenye kisiwa hiki”
“Huko ulikopita hadi umetokea
hapa, umeona nini?”
“Tumekuta nyumba hazina watu.
Pia tumekuta mafuvu na mifupa ya watu kila mahali”
“Basin a nyinyi ndio mtakuwa
hivyo hivyo, hamtapona”
Yale maneno yalinitisha na
kunifadhaisha.
“Yasmini kwanini unaniambia
hivyo. Mimi ni ndugu yako wa Zanzibar.
Hata katika harusi yako na mwana wa mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Moroco
nilialikwa na nilikuja Comoro lakini wewe ulitoweka katika mazingira ya ajabu.
Na leo ndio nakuona hapa” nikamwambia Yasmin kwa hofu.
“Nashukuru kwamba leo
nimetembelewa na ndugu yangu wa Zanzibar
na nashukuru kwamba umenijua lakini naona uchungu kuwa nitayashuhudia mauti
yako muda si mrefu”
>Kwanini unaniambia hivyo
Yasmin?. Niambie”
Yasmin bdala ya kunijibu
aliangua kilio.
Wenzangu mmoja mmoja wakaanza
kuingia mle chumbani na kushangaa kumuona yule msichana akilia.
“Je ni nani huyu?” Mmoja wa
wale wenzangu akaniuliza wakati wenzetu wengine walikuwa wamepigwa na butwaa.
“Ni msichana nimemkuta
amelala humu chumbani. Nilipoingia alizinduka na kuniambia anaitwa Yasmin. Ni
binti wa Rais wa Comoro” nikawaeleza.
“Ni binti wa Rais wa Comoro?”
Baadhi ya wenzangu wakaniuliza kwa mshangao. Walidhani labda nilikosea kusema.
“Ndiyo, mwenyewe ameniambia
hivyo na mimi pia namfahamu. Nilihudhuria katika harusi yake nchini Comoro
mwaka uliopita.
“Si ilisemekana kuwa yule
binti alitoweka?” Mmoja wa wenzangu akauliza.
“Ni kweli. Mimi pia
nimeshangaa kumkuta katika kisiwa hiki, tena akiwa peke yake. Na amenieleza
kitu cha kutisha”
“Kitu gani?”
“Mh! Ameniambia anaona
uchungu kuwa atayashuhudia mauti yetu muda si mrefu!”
Wenzangu wote wakashituka,
ndipo nilipojua kuwa hakuna mtu anayependa kufa.
“Kwanini amekwambia hivyo?”
Sautu za kuuliza zilisikika kutoka kwa wenzangu.
“Ndio nilikuwa namuuliza,
naona analia”
“Asilie, atueleze ili tujue…”
“Usilie dada yangu, nyamaza
utueleze ili tujue jinsi ya kujihami” nikamwambia msichan huyo.
“Pia atueleze jinsi
alivyofika katika kisiwa hiki cha ajabu” Mtu mwingine akasema.
itaendelea kesho.
Usikose mtu wangu
|
Saturday, December 6, 2014
Kisiwa cha Harishi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment