Monday, December 1, 2014

Maajabu na kweli


Hekaheka ya leo Desemba 01 inahusu yule Msichana Maua aliyepotea kupatikana.


Hekaheka ya leo Desemba 01 inahusu yule Msichana Maua aliyepotea kupatikana.

tunecast2
Kama hukusikiliza Hekaheka ya leo Jumatatu ya Desemba 01 kupitia Clouds Fm kwenye Leo Tena,  ni mwendelezo wa  Hekaheka ya Novemba 18 iliyokuwa  inahusu msichana Maua mwenye umri wa miaka 17 aliyepotea  siku ya Jumamosi Novemba 15.
Maua ambae alipotea wiki mbili zilizopita kama amerudi na kusema kuwa alikuwa Mbagala kwa Mpenzi wake Amiry ambaye alikutana naye njiani siku ambayo aliondoka kwao na kwenda kwa rafiki yake wa kiume, ambapo baada ya kuchelewa kurudi akahofia kwamba mama yake huenda angemkalipia, akaamua kwenda kwa Mchungaji  ambaye alimwambia arudi kesho yake ili afanyie maombi.
Kwa mujibu wa maelezo ya Maua anasema akiwa njiani alikutana na Amiry ambaye ni mlinzi wa Bar, na kumbembeleza ili waende kwake ambako amekuwa akiishi huko tangu usiku huo mpaka siku anayorudi nyumbani kwao.
Mama wa Maua amesema siku ambapo msichana huyo alikuwa anarudi alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Amiry na kumpa taarifa kwamba Maua atarudi siku hiyo.
Maua anasema aliongozana na Amiry lakini walipokaribia kwao aliamua kukimbia baada ya kikundi cha vijana kuanza kumzonga huku wakitishia kumkatama na baada ya hapo Amiry amekuwa akipigiwa simu na mama wa Maua ili aje waongee lakini imeonekana amekuwa akisita kutokana na hali aliyokutana nayo siku ya kwa mwanaume huyo   amekuwa akipigiwa Simu na Mama Maua ili waongee.
Taarifa ambazo zilifika Polisi usiku wa siku hiyo ni kwamba mama Maua alikutwa akihamisha vitu vyake bila kuaga hata majirani wakati bado kesi ya mtoto wake ikiwa haijaisha Polisi, ambapo Polisi waliikamata gari iliyopakia vitu hivyo huku sababu ya mama Maua kuhama bado haijafahamika.

Kumekucha blog inakupa matukio ya papo hapo, usipitwe peruzi kila wakati.

No comments:

Post a Comment