Kama ulipitwa na taarifa ya Habari ya ITV, ziko hapa zile story kubwa 3 ambazo nimekurekodia

Serikali ya Tanzania imesema msimamo
wake uko palepale sawasawa na msimamo wa nchi za Afrika ambapo kwa
pamoja wanapingana na utaratibu wa uendeshaji wa kesi za Mahakama ya ICC
licha ya Mahakama hiyo kumfutia mashtaka Rais Uhuru Kenyatta.
Akizungumza kuhusu msimamo huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema; “lakini
bado tunashikilia msimamo wetu ambao mwezi Januari tutautoa kwamba wala
hakuna sababu ya kudhalilisha viongozi wa Afrika na kuwanyanyasa kama
viongozi ambao ni watu tu wa kawaida au wahalifu mpaka mkawaburuza
kuwapeleka the Hague, hii kwakweli sisi hatuikubali… Wanatenda haki
lakini mchakato wenyewe wa kutenda haki unadhalilisha viongozi…”
MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA TANGA
Watu wawili wanaodhaniwa kuwa majambazi
wameuawa Tanga baada ya kuvamia kiwanda cha kusindika Chokaa na kufanya
jaribio la kupora fedha kiasi cha milioni 100 kutoka kwa Mhasibu wa
Kiwanda hicho.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki amesema; “majambazi
hao waliouawa ni Timoth Charles mkazi wa Mkwajuni Dar es Salaam, pamoja
na Mwinyimkuu Khamis mkazi wa Chanika, Dar es Salaam…”
Majambazi hao walikuwa wanne lakini wawili kati yao waliokuwa wamebaki nje walikimbia baada ya kushtuka kuwa wenzao wamebainika.
MELI YA Mv MAPINDUZI II KUWASILI Z’BAR
Meli ya Mv Mapinduzi II inatarajiwa
kuwasili mapema mwezi Januari visiwani Zanzibar kwa ajili ya majaribio
baada ya kununuliwa kutoka Korea Kusini ilipokuwa inaundwa.
Meli hiyo ambayo imenunuliwa na Serikali
ya Zanzibar kutokana na pato la kodi ina uwezo wa kubeba abiria 1,200
na tani 200 za mizigo.
Meli hiyo imegharimu kiasi cha dola milioni 30 mpaka kukamilika.
No comments:
Post a Comment